Lugha Nyingine
Maandamano ya kupinga NATO yafanyika kote nchini Sweden
Watu wakishiriki kwenye maandamano ya kupinga Sweden kuandaa mazoezi makubwa ya kijeshi ya kimataifa na nchi hiyo kuweka juhudi nyingi za kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) huko Stockholm, Sweden, Aprili 22, 2023. (Picha na Patrick Ekstrand/Xinhua)
STOCKHOLM - "NATO si lolote bali ni chombo cha vita cha Marekani," Nellie Puig, raia wa Sweden anayepinga nchi yake kujiunga na jumuiya hiyo ya kijeshi, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katikati mwa Stockholm siku ya Jumamosi.
Watu wakishiriki kwenye maandamano ya kupinga Sweden kuandaa mazoezi makubwa ya kijeshi ya kimataifa na nchi hiyo kuweka juhudi nyingi za kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) huko Stockholm, Sweden, Aprili 22, 2023. (Picha na Patrick Ekstrand/Xinhua)
"Siyo muungano wa kujihami kama wanavyodai. Ni shirika linaloendesha shughuli za Marekani," amesema Puig.
Maandamano ya kupinga Sweden kuandaa mazoezi makubwa ya kijeshi ya kimataifa na nchi hiyo kuweka juhudi nyingi za kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) yamefanyika katika miji 17 kote nchini humo siku ya Jumamosi.
Mashirika na mitandao kadhaa kama vile Jumuiya ya Amani na Usuluhishi ya Sweden, Hapana NATO, Hapana kwa Silaha za Nyuklia, na vyama vya kisiasa viliandaa maandamano hayo. Mamia walishiriki katika maandamano hayo huko Stockholm pekee.
Watu wakishiriki kwenye maandamano ya kupinga Sweden kuandaa mazoezi makubwa ya kijeshi ya kimataifa na nchi hiyo kuweka juhudi nyingi za kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) huko Stockholm, Sweden, Aprili 22, 2023. (Picha na Patrick Ekstrand/Xinhua)
Mabango yenye ujumbe kama vile "Hapana kwa NATO", "vita vya NATO vitafanya watoto wetu wauawe kwa dola moja," na "Zuia Aurora 23" -- ikirejelea mazoezi ya kijeshi yanayoendelea yakiwa na wanajeshi washiriki 26,000 hasa kutoka nchi wanachama wa NATO yanayoandaliwa kwa sasa na Sweden -- yalionekana wakati wa waandamanaji wakipita katikati ya jiji.
Mshiriki mwingine, Krister Holm, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Kikomunisti, ameliambia Xinhua kwamba Sweden itakuwa bora zaidi ikiwa haitachagua upande wowote.
"Itakuwa bora kwa maendeleo ya jamii, demokrasia, na utamaduni wa Sweden kama tutakuwa hatuegemei upande wowote. NATO ni muungano wa vita ambao unaweza kuiingiza Sweden kwenye mgogoro ambao hatutaki kuwa sehemu yake," amesema Holm ambaye pia ameitaka nchi yake kuendelea na sera ya kutotumia au kuunga mkono matumizi ya silaha za nyuklia.
Watu wakishiriki kwenye maandamano ya kupinga Sweden kuandaa mazoezi makubwa ya kijeshi ya kimataifa na nchi hiyo kuweka juhudi nyingi za kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) huko Stockholm, Sweden, Aprili 22, 2023. (Picha na Patrick Ekstrand/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma