Rais Xi Jinping wa China apokea hati za utambulisho za mabalozi 70 wanaoziwakilisha nchi zao China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2023

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba baada ya kupokea hati za utambulisho wa kitaifa za mabalozi 70 wanaoziwakilisha nchi zao nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 24, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

Beijing - Rais wa China Xi Jinping Jumatatu alipokea hati za utambulisho wa kitaifa za mabalozi 70 wanaoziwakilisha nchi, mashirika na maeneo yao nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Rais Xi pia alimpokea Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ushirikiano la Shanghai (SCO) Zhang Ming.

Akiwakaribisha mabalozi hao nchini China, Rais Xi amewataka kufikisha salamu za dhati na za mafanikio mema kwa viongozi wa nchi zao, viongozi wa mashirika na watu wa nchi zao.

Rais Xi amesema China iko tayari kuzidisha urafiki na kupanua ushirikiano wa kunufaishana na watu wa nchi nyingine mbalimbali kwenye msingi wa usawa na kunufaishana na kusukuma mbele uhusiano wa pande mbilimbili, na anatumai mabalozi hao watakuwa na uelewa wa pande zote na wa kina kuhusu China na kufanya kazi ya kuwa wajumbe wa urafiki na madaraja ya ushirikiano. Amesema, Serikali ya China itatoa usaidizi na urahisi kwa mabalozi hao kutekeleza majukumu yao.

Rais Xi pia ameelezea mapambano ya China dhidi ya UVIKO-19 yaliyoweka kipaumbele kwa watu na maisha yao, ametambua misaada ya nchi mbalimbali kwa China katika kukabiliana na janga hilo na mchango wa China wa kuchukua hatua madhubuti kuunga mkono kikamilifu mapambano ya kimataifa dhidi ya janga hilo.

Amesema, China imeanza safari mpya ya kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika mambo yote, na itahimiza Ustawishaji wa Taifa la China kupitia njia ya maendeleo ya kisasa ya China.

Amesisitiza kuwa China itaendelea kujitolea kwa njia ya maendeleo ya amani, kushikilia sera ya kitaifa ya kufungua mlango, kufuata kithabiti mkakati wa kunufaishana wa kufungua mlango, na kutoa fursa zaidi kwa Dunia kupitia maendeleo yake yenyewe.

Rais Xi amezikaribisha nchi na jumuiya ya kimataifa kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba baada ya kupokea hati za utambulisho wa kitaifa za mabalozi 70 wanaoziwakilisha nchi zao nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 24, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba baada ya kupokea hati za utambulisho wa kitaifa za mabalozi 70 wanaoziwakilisha nchi zao nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Aprili 24, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha