Simulizi ya Zawadi za Kitaifa za Rais Xi Jinping: Mtungi wa "Amani ya Dunia" wa mapambo ya Cloisonne

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2023

Mkutano wa 22 wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) ukifanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Ziwa Yanqi katika Eneo la Huairou la Beijing, Tarehe 11 Novemba, 2014. Rais wa China Xi Jinping aliongoza mkutano huo. (Picha/Lan Hongguang)

Mkutano usio rasmi wa 22 wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) ukifanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Ziwa Yanqi katika Eneo la Huairou la Beijing, Tarehe 11 Novemba, 2014. Rais wa China Xi Jinping aliongoza mkutano huo. (Picha/Lan Hongguang)

Mkutano usio rasmi wa 22 wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) ulifanyika kando ya Ziwa Yanqi, Beijing, Tarehe 11 Novemba, 2014.

Ili kuwakaribisha viongozi washiriki, Rais wa China Xi Jinping alichagua zawadi ya kitaifa kwa ajili yao, mtungi wa “Amani ya Dunia” wa mapambo ya Cloisonne, ambao ni sanaa ya jadi ya China. Ukomo wa kipenyo cha juu zaidi cha mtungi huo ni sentimita 21, ikiashiria makundi ya kiuchumi 21 ya APEC. Na michongo ya mawimbi ya maji kwenye mtungi huo wa rangi ya buluu ikiashiria eneo linalozunguka Bahari ya Pasifiki. Neno “mtungi” , tamshi lake la lugha ya Kichina ni sawa na tamshi la neno “Amani” la Kichina, kwa hivyo mtungi huo unaashiria amani ya dunia na kupata maendeleo kwa pamoja.

“Leo tunakusanyika kando ya Ziwa Yanqi ni kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, kufunga safari kwa pamoja, na kuandika ukurasa wa matarajio mapya ya maendeleo ya Asia-Pasifiki” alisema Xi Jinping.

Mtungi wa “Amani ya Dunia” ya mapambo ya Cloisonne, ambao ni  sanaa ya jadi ya China wa kuthamini (Picha/Hu Yang)

Mtungi wa “Amani ya Dunia” ya mapambo ya Cloisonne, ambao ni sanaa ya jadi ya China wa kuthamini (Picha/Hu Yang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha