Mji wa Wuxi wa China sehemu yenye maendeleo angavu kando ya Ukanda Mmoja, Njia Moja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2023

Sehemu ya Wuxi ya Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou inaenea kwenye eneo lenye urefu wa kilomita 41 huko Wuxi, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China.

Hapo zamani za kale, meli za wafanyabiashara zilisafirisha mchele, hariri na vigae kati ya maeneo ya Kusini na Kaskazini mwa China kupitia mfereji huo.

Leo, treni za mizigo zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya zinaondoka kwenye Stesheni ya Reli ya Wuxi Magharibi kuelekea Bara la Eurasia, zikisafirisha mashine za kufulia nguo, magari yanayotumia nishati ya umeme na bidhaa nyingine zinazotengenezwa nchini China hadi nchi zilizo kando ya Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Picha iliyopigwa kwa droni ikionyesha treni ya mizigo inayotoa huduma kati ya China na Ulaya ikiondoka kwenye Stesheni ya Reli ya Wuxi Magharibi, ikisafirisha bidhaa zinazotengenezwa nchini China kwenda nchi zilizo kando ya Ukanda Mmoja, Njia Moja. (Picha imepigwa kwa Droni/ Stesheni ya Usafirishaji ya Reli ya Wuxi Magharibi)

Kampuni ya Wuxi Little Swan, ambayo ni mtengenezaji mkuu wa mashine za kufulia nguo nchini China, ni mojawapo ya kampuni ambazo zimefaidika na huduma hiyo.

"Shukrani kwa huduma ya treni ya mizigo, tumepunguza gharama kwa asilimia 20 na kuboresha ufanisi kwa asilimia 30. Mwaka 2023, tunapanga kuongeza idadi ya makontena kwenye treni kwa asilimia 35," amesema Zhang Yan, Meneja Mkuu wa usafirishaji wa kampuni hiyo.

Kampuni ya Yadea ni kampuni inayoongoza kimataifa katika kuendeleza na kuunda pikipiki zinazotumia nishati ya umeme yenye makao yake makuu katika eneo la Xishan la Wuxi. Kampuni hiyo inamiliki vituo saba vya uzalishaji na mitambo 100 ya uzalishaji kote duniani na inauza bidhaa zake kwa nchi na kanda 100 duniani.

Picha iliyopigwa Machi, 2023 ikionyesha mojawapo ya mitambo ya uzalishaji ya Kampuni ya Yadea, ambayo ni kampuni inayoongoza kimataifa katika kuendeleza na kuunda pikipikizinazotumia nishati ya umeme. (Picha: Peng Yukai/People's Daily Online)

Eneo la Intaneti ya Magari (IoV) wa Wuxi, lililofunguliwa Agosti 2022, linakusanya pamoja zaidi ya kampuni 100 zinazoongoza, na kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo ya tasnia ya IoV nchini China.

Picha iliyopigwa Aprili, 2023 ikionyesha basi linalojiendesha lenyewe likifanya kazi katika Eneo la Intaneti ya Magari (IoV) wa Wuxi. (Picha: Liu Ning/People's Daily Online)

Picha iliyopigwa Aprili, 2023 ikionyesha basi linalojiendesha lenyewe likifanya kazi katika Eneo la Intaneti ya Magari (IoV) wa Wuxi. (Picha: Liu Ning/People's Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha