Maelfu ya watu wagongeana mayai na kuimba nyimbo katika kusherehekea Sikukuu ya Machi 3 ya Wilaya ya Dahua, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2023

IMG_256

Picha hii ikionyesha muonekano wa hali ya shughuli ya kugongeana mayai. (Picha na Li Hongying)

Asubuhi ya Aprili 22 Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wayao ya Dahua, Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, Kusini Magharibi mwa China ilifanya shughuli ya "Maelfu ya Watu Kugongeana Mayai na Maelfu ya Watu Kuimba Nyimbo" moja ya shughuli mfululizo za Wilaya ya Dahua za “Sikukuu ya Machi 3 ya Kabila la Wazhuang” kwenye kivutio cha Kilele Kizuri cha Eneo la Mandhari cha Kitongoji cha Yantan.

Inafahamika kwamba shughuli ya “Kugongeana Mayai” ni moja ya sehemu kuu za shughuli za kuimba nyimbo katika Sikukuu ya Machi 3 ya Kabila la Wazhuang, pia ni njia ya wavulana na wasichana kudhihirisha mapenzi yao. Wanawake na wanaume wa kabila la Wazhuang wanaoshiriki katika shughuli hiyo hugongeana mayai ya kuku au bata yaliyopakwa rangi nyekundu. Yule ambaye yai lake huvunjika anakuwa ameshindwa, na lazima atoe yai lake lililovunjika kwa mshindi na kumwimbia wimbo mmoja. Kila mwaka, vijana wengi wa kiume na wa kike huwa wapenzi kwenye shughuli hiyo katika Sikukuu ya Machi 3.

Siku hiyo pia, shughuli nyingine kama vile kuimba nyimbo za kienyeji na mashindano ya kubeba “bibi harusi” zilifanyika.

Wei Ruobin, Mkuu wa Kikundi cha Kikabila cha Nyimbo na Ngoma cha Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wayao ya Dahua, ameshiriki katika shughuli hiyo. Anasema: “shughuli ya ‘Machi 3’ ya maelfu ya watu kugongeana mayai” inaonyesha matarajio ya kila mmoja ya kufikia maisha bora ya watu. Ni yenye maana sana na inatakiwa kuirithiwa."

IMG_257

Picha hii ikionyesha mchezo wa kubeba “bibi harusi”. (Picha na Li Hongying)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha