Sikukuu ya Machi 3 yaonyesha mila na desturi mbalimbali za kabila la Wazhuang huko Wuming, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2023

Picha hii ikionyesha ufunguzi wa sherehe za sikukuu hiyo. (Picha na kituo cha vyombo vya habari cha Wuming)

Sikukuu ya Machi 3 ya mwaka huu imefika, ambayo inachukuliwa kama "Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China" ya pili na wenyeji wa Kitongoji cha Wuming wa Kabila la Wazhuang. Tamasha la Utalii wa Kitamaduni la Sikukuu ya Machi 3 ya Wuming ya 2023 lilifanyika kuanzia Aprili 20 hadi 23 huko Wuming, Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, Kusini Magharibi mwa China.

Kwenye hafla ya ufunguzi iliyofanyika mnamo Aprili 22, uwasilishaji maonyesho ya jukwaani, na mauzo ya vitu wakilishi vya urithi wa utamaduni usioshikika vyenye sifa za kikabila ni sehemu muhimu za hafla hiyo, pia ni kivutio kikubwa cha tamasha hilo la mwaka huu.

Shughuli nyingi zikiwemo maonyesho ya nyimbo na dansi za kijadi, maonyesho ya kumbukumbu za kitamaduni za kikabila, maonyesho ya mashindano ya michezo ya kijadi na maonyesho ya stadi za kijadi za kupika vyakula maalum vya kabila la Wazhuang zilifanyika kwenye hafla hiyo ya ufunguzi.

Picha hii ikionyesha onyesho la jukwaani la kupendeza. (Picha na Ma Xin)

Watu wakionyesha ustadi wa kijdaji: kupika “Ningmengya”, ambacho ni chakula kinachopikwa kwa kuchanganya nyama ya bata na limau. (Picha na Ma Xin)

Watu wakionyesha ustadi wa kijadi: kupika wali wa kunata wenye rangi tano. (Picha na Ma Xin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha