Mjumbe wa China katika Umoja wa Mataifa atoa wito wa kutekelezwa ushirikiano wa kweli wa pande nyingi

(CRI Online) April 25, 2023

Mjumbe wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametoa wito kwa nchi mbalimbali kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi.

Balozi Zhang amesema hayo alipohutubia Mjadala wa Wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kulinda Katiba ya Umoja wa Mataifa na ushirikiano wa pande nyingi.

Amesema hivi sasa jamii ya binadamu inakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazijawahi kutokea hapo zamani, vitendo vya umwamba vinaleta athari mbaya kwa dunia, na makundi ya kisiasa yanazusha mapambano na mivutano mikubwa, hivyo umuhimu wa kulinda Katiba ya Umoja wa Mataifa unazidi kuongezeka.

Balozi Zhang amesisitiza kuwa, China, ikiwa nchi mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama na nchi kubwa inayowajibika, inashikilia ushirikiano wa pande nyingi, na itahimiza kikamilifu utekelezaji wa mapendekezo ya maendeleo, usalama, na ustaarabu wa Dunia, kusukuma mbele maendeleo ya kisasa ya China, na kushiriki kikamilifu kazi ya Umoja wa Mataifa, ili kuchangia katika kuhimiza mshikamano na ushirikiano wa kimataifa, kukabiliana kwa pamoja na changamoto na kulinda thamani ya pamoja ya binadamu wote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha