Lugha Nyingine
Wakenya wang'ara katika Mbio za Marathon za Vienna na Hamburg
Wakenya wamejizolea ushindi katika mbio za marathon kwa wanaume na wanawake huko Vienna, Austria na Hamburg, Ujerumani siku ya Jumapili.
Samuel Mailu aliwaongoza wenzake sita na kutawala mbio za Marathon za Vienna huku Madgalyne Masai akiwa malkia wa mbio za wanawake.
Mailu alitumia saa mbili, dakika tano na sekunde nane kushinda, akiwaacha nyuma Bethwell Yegon na Titus Mutai walioshika nafasi za pili na tatu mtawalia. Masai alitumia saa 2:24:12, akimshinda mwanadada mwenzake Agnes Keino aliyekimbi mbio hizo kwa saa 2:24:25.
Nako kwenye mbio za Marathon za Hamburg nchini Ujerumani, Bernard Koech alitawala mbio hizo akishinda kwa kutumia muda wa saa 2:04:09 huku wenzake Joshua Belet (2:04:33) na Martin Kosgei (2:06:18) wakiibuka wa pili na wa tatu mtawalia.
Kwa upande wa wanawake Dorcas Tuitoek alitumia muda wa saa 2:20:09 na kujibebea taji akimshinda Tiruye Mesfin aliyeshika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa saa 2:20:18 huku Stella Chesang wa Uganda akiambulia nafasi ya tatu kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:20:23.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma