Guterres asema mfumo wa ushirikiano wa pande nyingi unakumbwa na shinikizo kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa

(CRI Online) April 26, 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 24 Aprili lilifanya mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu "Kulinda mfumo wa ushirikiano wa pande nyingi wenye ufanisi kupitia kufuata kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa", ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema mfumo wa ushirikiano wa pande nyingi unakumbwa na shinikizo kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Amesema kwa sasa hatua za ushirikiano wa pande nyingi zenye ufanisi zinahitajika zaidi katika kuzuia na kutatua migogoro, kusimamia hali ya sintofahamu katika maendeleo ya kiuchumi, na kulinda malengo ya maendeleo endelevu. Ushirikiano wa pande nyingi ni kiini cha Umoja wa Mataifa, pia ni sababu ya kuwepo kwa Umoja wa Mataifa na dhana ya mwongozo kwa umoja huo.

Ameongeza kuwa inapaswa kutafutwa njia ya kusonga mbele na kuchukua hatua mara moja, ili kuzuia migogoro na vurugu. Sasa ndio wakati wa kuhimiza ushirikiano, kuimarisha mashirika ya pande nyingi, na kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na changamoto za pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha