China yajibu kauli za Rais wa Korea ya Kusini kuhusu Mapambano ya Changjinhu

(CRI Online) April 30, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning Tarehe 28, Aprili alijibu kauli zilizotolewa na Rais wa Korea ya Kusini kuhusu mapambano ya Changjinhu ya Vita vya Korea kwenye mkutano wa kawaida na waandishi wa habari.

Msemaji Mao amesema, ushindi wa China katika vita vya Kuisaidia Korea dhidi ya Umwamba wa Marekani ulithibitisha kuwa, nchi yoyote au jeshi lolote likienda kinyume na mkondo wa kihistoria, na kuvamia nchi nyingine, hakika litapigwa vibaya.

Rais wa Korea ya Kusini Yoon Suk-Yeol ambaye alikuwa ziarani nchini Marekani alisema, vikosi vya Marekani vilipata ushindi mkubwa katika mapambano ya Changjinhu, wakati vilipokuwa vimezingirwa na vikosi vya China katika vita vya Kupinga Umwamba wa Marekani na Kuisaida Korea vilivyotokea miaka ya 50 karne iliyopita.

Msemaji Mao amesema, katika mapambano hayo, zaidi ya wanajeshi 24,000 wa Merakani waliangamizwa, na hata kamanda mmoja alikufa katika ajali wakati wa kutoroka, na Marekani inaona kuwa ilikuwa safari ndefu zaidi ya jeshi la Marekani ya kutoroka baada ya kushindwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha