Njia ya chini ya bahari yafunguliwa kwa matumizi ya umma katika Mji wa Dalian, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 02, 2023

Picha hii iliyopigwa Tarehe 30 Aprili 2023 ikionyesha handaki la barabara ya chini ya bahari huko Dalian, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Tarehe 30 Aprili 2023 ikionyesha handaki la barabara ya chini ya bahari huko Dalian, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua)

DALIAN - Njia ya chini ya bahari imefunguliwa kwa matumizi ya umma siku ya Jumatatu huko Dalian, mji wa pwani ulioko Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China.

Handaki hilo, lenye barabara mbili kila upande zenye njia sita za kupitisha magari chini ya Ghuba ya Dalian, ni handaki la kwanza lililozama chini ya bahari Kaskazini mwa China, amesema Sun Zhu, naibu mhandisi mkuu wa Kampuni ya Handaki la Chini ya Bahari la Ghuba ya Dalian, kampuni ambayo inasimamia ujenzi na uendeshaji wa handaki hilo.

Kasi iliyoundwa ya magari na vyombo vingine vya moto vya kusafiri katika handaki hilo lenye urefu wa kilomita 5.1 ni kilomita 60 kwa saa, amesema Sun. Ujenzi wa handaki hilo umechukua miaka minne hivi.

Barabara inayounganisha handaki hilo ilianza kufanya kazi siku ya Jumatatu, ikiunganisha pwani ya kaskazini na kusini mwa Ghuba ya Dalian, na kusaidia kupunguza msongamano wa magari na kupanua nafasi ya maendeleo ya mijini huko Dalian.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha