Mratibu wa misaada wa Umoja wa Mataifa ajitahidi kuendeleza operesheni za kibinadamu nchini Sudan

(CRI Online) Mei 02, 2023

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja huo Bw. Martin Griffiths na wadau wengine wanafanya kila juhudi kurejesha mwitikio wa kibinadamu kwa machafuko yanayoendelea nchini Sudan.

Msemaji huyo amesema Bw. Griffiths ametumwa kutafuta njia za kufikisha misaada ya kibinadamu kwa mamilioni ya watu ambao maisha yao yamevurugika kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Sudan.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, Bw. Griffiths sasa yuko Nairobi, Kenya ambako amekutana na Rais William Ruto wa Kenya, waziri wa mambo ya nje wa Canada Melenie Joly ambaye yuko ziarani nchini humo na wengine, ili kujadili hali tete nchini Sudan. Kwa hatua ijayo, Bw. Griffiths atajitahidi kuratibu na kuwezesha kuongeza misaada ya kibinadamu nchini Sudan.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha