Abiria nchini China waongezeka wakati wa likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 04, 2023

Picha hii iliyopigwa Tarehe 3 Mei 2023 ikionyesha abiria katika ukumbi wa kusubiri kupanda treni wa Stesheni ya Reli ya Shanghai Hongqiao huko Shanghai, Mashariki mwa China. China ilishuhudia kilele kipya cha usafiri huku idadi iliyokuwa ikiongezeka ya wasafiri wakiingia barabarani na kurejea kazini wakati ambapo likizo ya siku tano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi ikikamilika Jumatano. (Xinhua/Wang Xiang)

Picha hii iliyopigwa Tarehe 3 Mei 2023 ikionyesha abiria katika ukumbi wa kusubiri kupanda treni wa Stesheni ya Reli ya Shanghai Hongqiao huko Shanghai, Mashariki mwa China. China Jumatano ilishuhudia kilele kipya cha usafiri huku idadi iliyokuwa ikiongezeka ya wasafiri wakiingia barabarani na kurejea kazini wakati ambapo likizo ya siku tano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi ilikamilika. (Xinhua/Wang Xiang)

BEIJING –Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China siku ya Jumatano imekadiria kuwa idadi ya abiria iliyoshughulikiwa na mtandao wa usafirishaji wa kibiashara wa China wakati wa likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi inaweza kufikia zaidi ya wasafari milioni 270, au wastani wa kila siku wa wasafiri milioni 54.04, ikiwa ni ongezeko la asilimia 162.9 ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.

Wakati wa likizo hiyo ya siku tano iliyomalizika Jumatano, ikiwa ni likizo ya kwanza ya namna hiyo tangu China iboreshe hatua zake za kukabiliana na UVIKO-19, reli za China zinatarajiwa kushuhudia wastani wa kila siku wa safari za abiria milioni 18.18, ikiwa ni ongezeko la asilimia 464.4 kutoka likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi ya Mwaka 2022, imesema wizara hiyo.

Wastani wa kila siku wa mtiririko wa abiria kwa njia ya anga huenda ukafikia safari milioni 1.88, ambayo ni asilimia 507.4 zaidi ya kipindi kama hicho mwaka jana, wakati takwimu hizo za barabara kuu na njia za majini zinatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 99.1 na asilimia 114.2, mtawalia, wizara hiyo imesema.

Mtiririko wa abiria kwa njia ya barabara za mwendo kasi wakati wa likizo unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 101.83 hadi kufikia karibu safari milioni 62.1 kwa siku, kwa mujibu wa wizara hiyo.

Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China (MCT) Jumatano imesema, inakadiriwa kuwa safari za watalii wa ndani wakati wa likizo hiyo ziliongezeka kwa asilimia 70.83 kuliko kipindi hicho cha mwaka jana, na kufikia milioni 274,

Mapato yatokanayo na utalii yalifikia yuan bilioni 148.06 (sawa na dola bilioni 21.4 za Kimarekani), yakiwa ni ongezeko la asilimia 128.9 kutoka mwaka jana, kwa mujibu wa MCT.

Takriban shughuli 47,500 za kitamaduni na burudani zimefanyika kote nchini China, na karibu watu milioni 166 wameshiriki, imesema MCT.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha