Russia yasema Washington inahusika na shambulio la droni dhidi ya Ikulu ya Kremlin

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 05, 2023

Ishara ya "Hakuna Ruhusa ya Ndege Kuruka" ikionekana karibu na Ikulu ya Kremlin huko Moscow, Russia, Mei 3, 2023. (Picha na Alexander Zemlianichenko Jr/Xinhua)

Ishara ya "Hakuna Ruhusa ya Ndege Kuruka" ikionekana karibu na Ikulu ya Kremlin huko Moscow, Russia, Mei 3, 2023. (Picha na Alexander Zemlianichenko Jr/Xinhua)

MOSCOW/WASHINGTON - Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema Alhamisi kuwa Russia ina ushahidi unaoonyesha kwamba Marekani na Ukraine zilihusika na shambulio la hivi majuzi la droni kwenye Ikulu ya Kremlin.

"Tuna data hii. Data ambayo imepokelewa na kikosi chetu maalum," Peskov amesema kuhusu jaribio la shambulio la droni lililofanyika Jumatano kwenye Ikulu ya Kremlin.

Peskov ameeleza kuwa Marekani lazima ielewe kwamba Russia inafahamu ushiriki wake katika shambulio la kigaidi, akisema kwamba ni muhimu kwa Washington "kuelewa jinsi ushiriki huo wa moja kwa moja katika mgogoro ulivyo hatari."

Idara ya Habari ya Ikulu ya Russia ilisema Jumatano kwamba Ukraine ilijaribu kumuua Rais wa Russia Vladimir Putin kwa kutumia droni mbili kushambulia makazi yake ya Kremlin.

Ikulu ya Kremlin ilisema jeshi na kikosi maalum vilitumia rada za kivita kuzima droni hizo.

Wakati huo huo, Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani John Kirby amesema Alhamisi kwamba madai ya Russia ni ya uongo. Ameviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa "hakuna kuhusika kwa Marekani" katika shambulio hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha