Serbia na China zaadhimisha kumbukumbu ya miaka 24 tangu NATO ilipolipua ubalozi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2023

https://english.news.cn/20230507/c5df7b9082cb4250940823207e30f1ac/85afbd4f34a84435bd55605661feebbf.jpg

Wawakilishi kutoka makampuni ya biashara ya China wakiomboleza mbele ya mnara wa ukumbusho kwenye eneo la Ubalozi wa zamani wa China katika Jamhuri ya Shirikisho ya Yugoslavia huko Belgrade, Serbia, Mei 7, 2023. (Xinhua/Ren Pengfei)

https://english.news.cn/20230507/c5df7b9082cb4250940823207e30f1ac/268dfa0398e4444196d159f6b8e1831d.jpg

Watu wakiwa wameshikilia maua wakiomboleza waathirika kwenye eneo la Ubalozi wa zamani wa China katika Jamhuri ya Shirikisho ya Yugoslavia huko Belgrade, Serbia, Mei 7, 2023. (Xinhua/Ren Pengfei)

https://english.news.cn/20230507/c5df7b9082cb4250940823207e30f1ac/6541674afa614db7af060ee62287b75c.jpg

Wawakilishi kutoka makampuni ya biashara ya China wakiinama mbele ya mnara wa ukumbusho kwenye eneo la Ubalozi wa zamani wa China katika Jamhuri ya Shirikisho ya Yugoslavia huko Belgrade, Serbia, Mei 7, 2023. (Xinhua/Ren Pengfei)

https://english.news.cn/20230507/c5df7b9082cb4250940823207e30f1ac/13651d80d9c748c0b78c13bb645b4c9f.jpg

Waziri wa Michezo wa Serbia Zoran Gajic na Balozi wa China nchini Serbia Chen Bo wakiomboleza mbele ya mnara wa ukumbusho kwenye eneo la Ubalozi wa zamani wa China katika Jamhuri ya Shirikisho ya Yugoslavia mjini Belgrade, Serbia, Mei 7, 2023. (Xinhua/Ren Pengfei)

BELGRADE - Waserbia na Wachina walikusanyika kwenye eneo la Ubalozi wa zamani wa China katika Jamhuri ya Shirikisho ya Yugoslavia huko Belgrade siku ya Jumapili kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 24 ya mauaji ya waandishi wa habari watatu wa China kwenye uvamizi wa Mwaka 1999 uliofanywa na Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) dhidi ya Yugoslavia.

Balozi wa China nchini Serbia Chen Bo, Waziri wa Michezo wa Serbia Zoran Gajic, pamoja na maafisa na raia mbalimbali waliweka mashada na maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya waathirika - Shao Yunhuan wa Shirika la Habari la China, Xinhua, na Xu Xinghu na mkewe Zhu Ying wa gazeti la Guangming Daily.

Gajic amesema kuwa shambulio dhidi ya Ubalozi wa China ni kitendo cha woga kilichofanywa na wavamizi wa NATO, "ili kupanda mbegu ya uovu."

Kwa upande wake Balozi Chen amesema kwamba mashujaa wa shambulio la bomu "waliuawa kikatili," lakini miaka 24 baadaye, mwelekeo unaokua wa maendeleo ya amani unaleta matumaini kwa binadamu.

"Miaka 24 imepita, hali ya kimataifa imekuwa na mabadiliko makubwa, na China na Dunia pia imepitia mabadiliko ya kutikisa. Ingawa siasa za madaraka na umwamba bado ndiyo sababu kuu za msukosuko wa Dunia ya leo, nguvu zinazojitolea kufanya maendeleo ya amani zinazidi kuimarika na kuimarika,” amesema.

Mei 7, 1999, vikosi vya NATO vinavyoongozwa na Marekani vilifanya shambulio la kikatili la kombora kwenye Ubalozi wa zamani wa China huko Belgrade, ambalo lilisababisha vifo vya waandishi wa habari watatu wanaofanya kazi huko, zaidi ya watu 20 kujeruhiwa, na jengo la ubalozi kubomolewa vibaya.

Mahali pa jengo hilo la ubalozi lililoharibiwa sasa kuna Kituo kipya cha Utamaduni cha China, kinachoangalia minara miwili ya ukumbusho wa mauaji hayo ya kikatili yaliyotokea hapa miaka 24 iliyopita. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha