Makamu wa Rais wa China ashiriki kwenye sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charles III

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2023

Makamu wa Rais wa China Han Zheng, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, akihudhuria sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa Uingereza na shughuli nyingine zinazohusika  baada ya kualikwa, mjini London, Uingereza, kuanzia Mei 5 hadi Mei 6, 2023. (Xinhua)

LONDON - Makamu wa Rais wa China aliyezuru Uingereza Han Zheng alishiriki kwenye sherehe ya kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa Uingereza na shughuli nyingine zinazohusika baada ya mwaliko kutoka Mei 5 hadi Mei 6.

Han, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, aliwasilisha kwa Mfalme Charles III salamu za Rais Xi za pongezi za dhati na kumtakia heri mfalme na Malkia Camilla, familia ya kifalme ya Uingereza na watu wa Uingereza, na kushukuru upande wa Uingereza kwa uratibu makini wa ziara yake nchini humo.

Mfalme Charles III alimwomba Han kuwasilisha shukrani zake za dhati na salamu zake za dhati kwa Rais Xi, amemshukuru Rais Xi na mkewe Profesa Peng Liyuan kwa kutuma salamu za pongezi kwake na kwa Malkia, na kumkaribisha Han akiwa ni mwakilishi maalum wa Rais Xi kushiriki kwenye sherehe za kutawazwa.

Mfalme Charles III akibainisha kuwa uhusiano kati ya Uingereza na China ni muhimu sana, ameeleza matumaini yake kuwa nchi hizo mbili zitafanya ushirikiano zaidi katika nyanja mbalimbali kama vile maendeleo ya kijani na utoaji kaboni chache, maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabianchi, na anatazamia China itaendelea kutoa mchango mkubwa wa kiuongozi katika maendeleo ya kijani na nyanja nyingine.

Katika ziara yake hiyo, Han pia alikuwa na mikutano mifupi na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, Mwanamfalme wa Wales William, na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu Oliver Dowden.

Huku Han akipongeza kwamba ushirikiano kati ya China na Uingereza una msingi mzuri na uwezo mkubwa, amesema katika zama za mafungamano, uchumi wa nchi mbalimbali umeunganishwa kwa kina, "China inaendelea kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu na itahimiza zaidi kufungua mlango kwenye kiwango cha juu, na iko tayari kuimarisha ushirikiano na upande wa Uingereza kwa manufaa ya pande zote na kupata maendeleo kwa pamoja."

Mei 4, Han alishiriki kwenye hafla ya kukaribishwa ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na jumuiya ya wafanyabiashara wa China na Uingereza huko London.

Makamu wa Rais Han alipongeza nafasi muhimu na juhudi za jumuiya ya wafanyabiashara wa Uingereza katika kuhimiza mabadilishano na ushirikiano na China, akieleza matumaini kwamba jumuiya hiyo itaendelea kuchangia hekima na nguvu katika kuendeleza uhusiano wa pande hizo mbili. 

Makamu wa Rais wa China Han Zheng, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, akihudhuria sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa Uingereza na shughuli nyingine zinazohusika  baada ya kualikwa, mjini London, Uingereza, kuanzia Mei 5 hadi Mei 6, 2023. (Xinhua)

Makamu wa Rais wa China Han Zheng ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Oliver Dowden mjini London Uingereza. (Xinhua/Li Tao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha