China, Afghanistan na Pakistan zaahidi kuimarisha ushirikiano katika masuala ya usalama na kupambana na ugaidi

(CRI Online) Mei 08, 2023
China, Afghanistan na Pakistan zaahidi kuimarisha ushirikiano katika masuala ya usalama na kupambana na ugaidi

China, Afghanistan na Pakistan zimeahidi kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande tatu kuhusu usalama na kupambana na ugaidi.

Akihudhuria Mazungumzo ya Mawaziri wa Mambo ya Nje na wenzake wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardari na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya mpito ya Afghanistan Amir Khan Muttaqi, huko Islamabad Pakistan juzi Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Qin Gang alisema zikiwa nchi jirani zenye urafiki wa jadi, China iko tayari kufanya juhudi pamoja na Afghanistan na Pakistan kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Dunia, Mpango wa Usalama wa Dunia na Mpango wa Ustaarabu wa Dunia.

Amebainisha kuwa China iko tayari kutumia kwa pamoja fursa za maendeleo na kukabiliana na changamoto za kiusalama na nchi hizo mbili ili kuweka mfano wa ushirikiano kwa majirani zao, na kushughulikia masuala ya pande nyingi na kikanda kupitia mifumo ya pande mbili na tatu.

Kwa upande wao Muttaqi na Bilawal wamesema ushirikiano kati ya China, Afghanistan na Pakistan una umuhimu mkubwa kwa amani na ustawi wa kikanda, na kuahidi kuwa ziko tayari kukuza ushirikiano wa pande tatu, kuandaa mwongozo wa ushirikiano katika nyanja kama vile siasa, usalama na uchumi, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi hizo tatu, kufikia manufaa ya pamoja na matokeo ya kunufaishana, na kuzinufaisha nchi hizo tatu jirani na nchi nyingine za kanda hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha