Syria yajiunga tena na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu baada ya kutokuwepo kwa miaka 12

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2023

https://english.news.cn/20230507/357e786fbfa64364b8df55c7d3591c53/da3d53937a684254b75ee4ed1a09c42a.jpg

Picha hii iliyopigwa Mei 7, 2023 ikionyesha eneo la mkutano maalum wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) uliofanyika Cairo, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

CAIRO - Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu wameamua katika mkutano maalum wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) uliofanyika Cairo Jumapili kurejesha uanachama wa Syria katika jumuiya hiyo baada ya kusimamishwa uanachama kwa miaka 12, imesema taarifa ya mwisho baada ya mkutano huo.

Mkutano wa baraza la AL katika ngazi ya mawaziri umeamua kuanzisha tena "ushiriki wa wajumbe wa serikali ya Syria katika mikutano ya baraza la AL na mashirika na vyombo vyake vyote kuanzia Mei 7, 2023," inasomeka taarifa hiyo iliyotolewa.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu pia wamekubaliana juu ya umuhimu wa kuongeza juhudi "kuisaidia Syria kutoka katika mgogoro wake."

Wametangaza kufanya juhudi zao mpya za "kuhifadhi mamlaka, umoja wa ardhi, utulivu, na uadilifu wa kikanda wa Syria kwa kuzingatia mkataba wa AL na kanuni zake," kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Kurejeshwa uanachama wa Syria katika AL ndilo lililokuwa kiini cha mkutano wa wiki jana kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Jordan, Saudi Arabia, Iraq, Misri na Syria katika mji mkuu wa Jordan, Amman.

Mazungumzo hayo ya Amman yalikuwa ni sehemu ya mpango ulioongozwa na Jordan kwa ajili ya kurejesha kawaida uhusiano wa AL na Syria ambayo uanachama wake wa AL ulisitishwa Mwaka 2011.

Siku chache baada ya mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Prince Faisal bin Farhan Al Saud alifanya ziara huko Damascus, ikiwa ni ziara ya kwanza ya afisa wa Saudi nchini Syria katika kipindi cha miaka 12. 

https://english.news.cn/20230507/357e786fbfa64364b8df55c7d3591c53/e319951d099f42c2aad34c21e4b294a9.jpg

Picha hii iliyopigwa Mei 7, 2023 ikionyesha bendera ya Taifa la Syria (ya nne kushoto) kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) huko Cairo, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

https://english.news.cn/20230507/357e786fbfa64364b8df55c7d3591c53/58cd23474ef1412ea7b8da4b2c5ecbe3.jpg

Picha hii iliyopigwa Mei 7, 2023 ikionyesha eneo la mkutano maalum wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) uliofanyika Cairo, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

https://english.news.cn/20230507/357e786fbfa64364b8df55c7d3591c53/cf2cf74352114ceeae0a7cfd709ce321.jpg

Picha hii iliyopigwa Mei 7, 2023 ikionyesha eneo la mkutano maalum wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) uliofanyika Cairo, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha