China yafuata maendeleo yenye ubora wa hali ya juu ya idadi ya watu ili kusaidia maendeleo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2023

Wanafunzi kutoka Shirikisho la Ndege za Mfano la Taasisi ya Teknolojia ya Harbin wakirusha ndege za mfano kwenye kampasi ya Harbin, Mji Mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini-Mashariki mwa China, Aprili 22, 2023. (Xinhua/Xie Jianfei)

Wanafunzi kutoka Shirikisho la Ndege za Mfano la Taasisi ya Teknolojia ya Harbin wakirusha ndege za mfano kwenye kampasi ya Harbin, Mji Mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini-Mashariki mwa China, Aprili 22, 2023. (Xinhua/Xie Jianfei)

BEIJING - China imetoa ishara wazi ya kuendana na kukabiliana na hali mpya ya kawaida katika idadi ya watu katika jitihada za kuendeleza maendeleo ya kisasa kwa kuboresha sifa ya jumla ya idadi ya watu wake.

Kwa mujibu wa mkutano wa Kamati Kuu ya Mambo ya Fedha na Uchumi ya China uliofanyika wiki iliyopita, China hivi sasa inakabiliwa na hali ya kupungua kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa, kuzeeka kwa idadi ya watu, na tofauti katika ukuaji wa idadi ya watu kwa mikoa yake.

Takwimu mpya zilizotolewa zinaonyesha kuwa idadi ya jumla ya watu wa China ilifikia bilioni 1.41175 mwishoni mwa Mwaka 2022, ikiwa ni kushuka kwa idadi ya watu 850,000 kutoka mwisho wa Mwaka 2021.

"Kupungua kidogo kwa idadi ya watu na jamii inayozidi kuzeeka ni jambo lisiloepukika wakati wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii," amesema He Dan, Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Idadi ya Watu na Maendeleo cha China.

Lakini China bado ni tajiri kwa utoaji wa nguvu kazi, kutokana na kuwa na idadi ya watu wake inayofikia bilioni 1.4. Kando na hilo, idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi nchini China inakaribia milioni 900, na milioni 15 zaidi wanajiunga na nguvu kazi kila mwaka.

Wakati huo huo, mgao wa talanta wa China, kama matokeo ya mchango zaidi wa elimu, unakua. Zaidi ya watu milioni 240 kote nchini China wamepata elimu ya juu. Idadi ya wafanyakazi wa utafiti na maendeleo nchini China iko juu zaidi duniani.

Ili kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China, mkutano huo wa wiki jana ulisema China inapaswa kuharakisha maendeleo ya rasilimali watu ya kisasa yenye ubora mzuri, wingi wa kutosha, muundo ulioboreshwa, na ugawaji unaokubalika.

Mkutano huo umesisitiza kufanya juhudi zaidi za kudumisha kiwango kinachofaa cha kuzaliwa watoto na kiwango cha idadi ya watu. China itaendeleza huduma shirikishi za malezi ya watoto, kupunguza mzigo kwa familia zenye kulea watoto, malezi kwa watoto na elimu, na kuhimiza ujenzi wa jamii yenye kupenda kuzaa watoto, kwa mujibu wa mkutano huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha