Mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) ya China yaongezeka kwa asilimia 85.6 Mwezi Aprili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2023
Mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) ya China yaongezeka kwa asilimia 85.6 Mwezi Aprili
Wageni wakichunguza jukwaa la magari yanayotumia nishati mpya (NEV) la Kampuni ya Magari ya Cadillac kwenye Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Tasnia ya Magari ya Shanghai huko Shanghai, Mashariki mwa China, Aprili 18, 2023. (Xinhua/Fang Zhe)

BEIJING - Mauzo ya rejareja ya magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) nchini China yameongezeka kwa asilimia 85.6 Mwezi Aprili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, takwimu kutoka Shirikisho la Magari ya Abiria la China (CPCA) zimeonyesha Jumanne.

Jumla ya magari yanayotumia nishati mpya 527,000 yameuzwa nchini China mwezi uliopita, ikiwa ni kiwango cha chini kwa asilimia 3.6 kutoka Machi, kwa mujibu wa CPCA.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya ya chapa kuu za China yamechukua asilimia 70.5 ya jumla ya mauzo yote ya magari hayo.

China imeuza nje magari 91,000 ya abiria yenye kutumia nishati mpya mwezi uliopita, ikiwa ni kuongezeka kwa asilimia 1,028.5 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana na kuongezeka kwa asilimia 29.4 ikilinganishwa na Machi.

Katika miezi minne ya kwanza ya mwaka, mauzo ya rejareja ya magari yanayotumia nishati mpya nchini China yalipanda kwa asilimia 36 hadi kufikia magari milioni 1.84 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, CPCA imesema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha