Lugha Nyingine
Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Ulinzi wa Ndege 8 za kivita “Dragoni Mkali”
Picha ya kwanza: picha hii ikionyesha ndege 8 za kivita “Dragoni Mkali” kulinda ndege ya Rais Xi, picha ambayo ni zawadi waliyotoa viongozi wa Pakistani kwa Rais Xi. (Picha na Hu Yang)
Katika zawadi za kitaifa alizopokea Rais Xi Jinping wa China, kuna picha maalum --- Ndege maalum yenye alama ya bendera ya taifa ya China, ambayo nyuma yake kuna ndege 8 za kivita "Dragoni Mkali" za Pakistan zilizojipanga kwa pande mbili kwa ajili ya kulinda ndege ya rais Xi. Hii ni heshima ya juu ya kumkaribisha rais Xi aliyekwenda ziarani nchini Pakistani mwezi Aprili, 2015.
Kwa nini Pakistani ilichagua ndege za kivita za “Dragoni Mkali” kufanya ulinzi huo? Kwa sababu ndege za aina hiyo ni udhihirisho wa ushirikiano wa China na Pakistani. Katika miaka ya 1990, Pakistani ilitaka kushirikiana na China kuunda ndege ya kivita ya hali ya juu. Mwaka 2003, ndege ya kivita "Dragoni Mkali" iliyoundwa kwa juhudi kubwa sana za wataalam wa nchi hizo mbili ilifaulu kufanya safari yake ya kwanza. Utendaji bora wa Ndege ya kivita “Dragoni Mkali” umehakikisha kwa nguvu usalama wa Taifa la Pakistani, hivyo umesifiwa na jeshi la Pakistani kuwa ni "mradi wa ushirikiano wenye mafanikio zaidi kati ya China na Pakistani".
Katika wakati wa ziara hiyo, Rais Xi na viongozi wa Pakistani waliamua kupandisha ngazi ya uhusiano wa China na Pakistani , na kutaja uhusiano huo kuwa ni "uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati " wa siku zote, inamaanisha daima kusonga mbele pamoja bila kujali tatizo lolote na changamoto yoyote.
Picha ya pili: Aprili 21, 2015, Rais Xi Jinping alitoa hotuba muhimu yenye kauli mbiu ya “Kujenga jumuiya ya China na Pakistani yenye mustakabali wa pamoja na kufunga safari mpya ya ushirikiano wa kunufaishana ” kwenye Bunge la Pakistani. (Picha na Yao Dawei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma