Maeneo ya Biashara Huria ya China yashuhudia ukuaji thabiti miezi ya Januari-Machi mwaka huu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2023

Picha hii iliyopigwa Tarehe 21 Juni 2022 ikionyesha Eneo la Majaribio la Biashara Huria (FTZ) la China huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)

Picha hii iliyopigwa Tarehe 21 Juni 2022 ikionyesha Eneo la Majaribio la Biashara Huria (FTZ) la China huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)

BEIJING - Maeneo ya Biashara Huria ya China yamerekodi ukuaji wa kasi wa biashara na uwekezaji wa nje katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, imesema Wizara ya Biashara ya China siku ya Alhamisi.

Jumla ya thamani ya biashara ya nje ya Maeneo 21 ya Biashara Huria ya China ilifikia yuan trilioni 1.8 (kama dola za kimarekani bilioni 260.5) katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.6 kuliko ile ya mwaka uliopita , amesema msemaji wa wizara hiyo Shu Jueting kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Shu amesema kiwango hiki cha ukuaji kilikuwa ni asilimia 1.8 zaidi ya kiwango cha kitaifa.

Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kwenye maeneo hayo ya biashara huria katika matumizi halisi uliongezeka kwa asilimia 22.1 kuliko mwaka jana hadi kufikia thamani ya yuan bilioni 71.9, msemaji huyo amesema.

Shu amesema, maeneo hayo ya biashara huria kwa nchi nzima ya China yamefanya juhudi za pande nyingi ili kukuza biashara na uwekezaji wa nje, ikiwa ni pamoja na kuhimiza uvumbuzi wa kitaasisi, kuongeza uungaji mkono kwa shughuli zenye nguvu bora, kuboresha huduma, na kuongeza ufanisi katika usambazaji wa bidhaa.

Shu ameongeza kuwa wizara hiyo itaandaa shughuli mbalimbali kusaidia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kujifunza zaidi kuhusu sera za Maeneo ya Biashara Huria ya China na kunufaika pamoja na fursa ya maendeleo ya baadaye.

China ilianzisha eneo lake la kwanza la biashara huria huko Shanghai Mwaka 2013.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha