Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa atoa wito wa msamaha wa madeni kwa nchi zenye uchumi wa kipato cha kati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2023

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Korosi akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu nchi zenye uchumi wa kipato cha kati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 11, 2023. Korosi siku ya Alhamisi ametoa wito wa msamaha wa madeni, pamoja na upatikanaji sawa wa teknolojia mpya, kwa nchi zenye uchumi wa kipato cha kati. (Loey Felipe/Picha ya UN/ Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Korosi siku ya Alhamisi alitoa wito wa msamaha wa madeni, pamoja na upatikanaji sawa wa teknolojia mpya, kwa nchi zenye uchumi wa kipato cha kati.

Ameuambia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu nchi zenye uchumi wa kipato cha kati kwamba, nchi 110 zenye uchumi wa kipato cha kati, ambazo huchukua robo tatu ya idadi ya watu wote duniani na karibu theluthi moja ya Pato la Dunia, ni vichocheo vikuu vya maendeleo ya kimataifa.

"Jiografia, mifumo ya ikolojia, utamaduni na uchumi wenu ni anuai sana -- na udhaifu tofauti. Baadhi yenu hukumbana na ukame wa mara kwa mara na kutoweka kwa misitu kunakoleta majangwa, huku wengine mnakabiliwa na dhoruba za kitropiki na kupanda kwa kina cha bahari. Lakini nyote mnakabiliwa na changamoto ya pamoja ya kujenga uwezo wenu wa kukabiliana na hali hizi mbaya kwa njia zinazohakikisha uhimilivu" amesema.

Korosi amesema ni wakati wa kuweka msisitizo kuhusu msamaha wa madeni kwa nchi zenye uchumi wa kipato cha kati, ambazo ni nyumbani kwa watu wengi maskini zaidi duniani.

Amesema, hatua mbalimbali za misamaha ya madeni zinaweza kuzingatiwa. Mabadilishano ya deni kwa mabadiliko ya tabianchi au deni kwa mazingira asilia yanatoa faida za pande zote kwa wadaiwa, wadai na wafadhili ili kufikia malengo ya maendeleo ya kitaifa kwa kuendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Amebainisha kuwa Mfuko wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wa Uhimilivu na Uendelevu na Dirisha la upungufu wa Chakula, pamoja na Mfuko wa hasara na uharibifu uliokubaliwa kwenye Mkutano wa hivi karibuni wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi nchini Misri, unafungua njia za kupanua ufadhili wa dharura kwa nchi zinazohitaji.

“Nchi zenye uchumi wa kipato cha kati zinahitaji upatikanaji sawa wa teknolojia, sayansi na uvumbuzi mpya ambao huchochea uhimilivu kwa muda mrefu,” amesema Korosi.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Korosi (katikati mezani na kwenye skrini) akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu nchi zenye uchumi wa kipato cha kati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 11, 2023. (Loey Felipe/Picha ya Umoja wa Mataifa/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha