Kuishi vijijini kwapata umaarufu miongoni mwa wakazi wa mijini wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 15, 2023

Mtalii akitembea karibu na hosteli iliyopo Kijiji cha Qianyuan katika Mji wa Jiande, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Februari 28, 2023. (Xinhua/Xu Yu)

Mtalii akitembea karibu na hosteli iliyopo Kijiji cha Qianyuan katika Mji wa Jiande, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Februari 28, 2023. (Xinhua/Xu Yu)

BEIJING - Wakati wa likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi mwaka huu, mkazi anayetumia jina la ubini la Yao aliihudumia familia yake kwa mapumziko tulivu katika eneo la nje ya Mji wa Beijing, China. Familia hiyo ilichagua jumba la kupendeza la kukodisha kwa muda mfupi lililopo katikati ya milima, ambalo lipo umbali wa kama dakika 90 kwa gari kutoka nyumbani kwao katika eneo la katikati mwa Mji wa Beijing, China.

"Ilihisi kama kuishi katikati ya mchoro, mbali na maeneo ya vivutio vya watalii yaliyojaa," Yao alisema.

Hapo awali, kijiji hiki cha mbali cha milimani katika Eneo la Miyun la Beijing kilikumbwa na msongamano wa magari na maendeleo kudorora. Wakati Fulani huko nyuma, hata huduma za kimsingi kama vile maduka madogo hazikuwepo kijijini.

Mabadiliko makubwa yalianza kujitokeza Mwaka 2022 wakati kijiji kilipotekeleza mradi wa uwekezaji wenye lengo la kukarabati makazi yenye kuenea eneo lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 3,000. Matokeo yake, mapato na matumizi ya wanakijiji yalishuhudia ongezeko kubwa, na kusababisha wimbi la maendeleo mapya ndani ya kijiji hicho kilichojitenga cha milimani.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mwelekeo unaokua miongoni mwa wakazi wa mijini wa China wa kukumbatia mtindo mpya wa maisha kwa kuchagua kuishi katika maeneo ya vijijini. Mabadiliko haya yamesababisha ustawishaji wa vijiji vya milimani na kukarabatiwa kwa kufanya upya kwa nyumba za vijijini zilizotelekezwa, na kuleta pumzi mpya ya uhai katika ardhi ya vijijini iliyopuuzwa hapo awali.

Jukwa la "Meilixinxiangcun," ambalo ni jukwaa la mtandaoni mahsusi kwa ajili ya ukodishaji wa nyumba za vijijini nchini China, hutoa aina mbalimbali za nyumba zisizo na wakazi ndani yake zilizo katika maeneo ya vijijini kote China. Kwa mujibu wa timu ya huduma kwa wateja ya jukwaa hilo, muda wa kukodisha nyumba hizi unaweza kuanzia miezi michache hadi miongo kadhaa, na kodi ya kila mwaka inatofautiana kutoka yuan 10,000 (kama dola 1,440 za Marekani) hadi makumi ya maelfu ya yuan.

Matarajio ya kukarabati kibinafsi nyua na nyumba za vijini yameibuka kuwa matamanio ya kuthaminiwa kwa wakaazi wengi wa mijini.

Mkazi wa Shanghai, anayetumia jina la "Zhanzhan" kwenye mtandao wa kijamii wa Xiaohongshu nchini China unaohusika na watu kushiriki mitindo ya maisha, ameshiriki video za kuvutia za safari yake ya ukarabati wa nyumba na uwa wake kwenye ukurasa wake wa mtandaoni, na kuvutia idadi kubwa ya maoni ya watumiaji wa mtandao.

Katika muda wa siku mbili, video yake ya kuvutia iliyochapisha kazi yake ngumu ya mwaka mzima ya ukarabati wa makazi ya vijijini ilisambaa, na hivyo kufanya idadi ya wafuasi wake mtandaoni kuongezeka kutoka 3,000 hadi 50,000.

Video yake imeweza kuvutia hisia za vijana wengi na baadhi yao pia wamehamasishwa na yeye kuishi kijijini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha