Mkutano wa Viongozi Wakuu wa China na Nchi za Asia ya Kati ni hatua muhimu katika kuhimiza utulivu wa kikanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 15, 2023

Picha hii iliyopigwa Tarehe 25 Aprili 2023 ikionyesha mandhari ya Lango la Yongning la ukuta wa mji wa kale wa Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China. (Xinhua/Liu Xiao)

Picha hii iliyopigwa Tarehe 25 Aprili 2023 ikionyesha mandhari ya Lango la Yongning la ukuta wa mji wa kale wa Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China. (Xinhua/Liu Xiao)

BISHKEK - Mkutano ujao kati ya viongozi wakuu wa China na nchi za Asia ya Kati utafungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya China na nchi za Asia ya Kati na kuhimiza utulivu na maendeleo ya kikanda, Nurzhan Kasmalieva, mkuu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Jimbo la Kabar nchini Kyrgyzstan, amesema.

China na nchi za Asia ya Kati zitafanya mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana wa ngazi ya juu, ambao unaonesha ushirikiano thabiti kati ya China na nchi tano za Asia ya Kati, Kasmalieva ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano Alhamisi.

"Ugaidi na itikadi zenye mrengo mkali ni tishio na changamoto kwa usalama wa Asia ya Kati wakati wowote, na ninatumai kuwa matokeo zaidi ya ushirikiano wa kiusalama yanaweza kupatikana katika mkutano huo, ili kuhimiza usalama na utulivu katika eneo hilo," amesema.

Huku akibainisha kuwa ustawi wa kiuchumi ni sharti la amani na utulivu, na mkutano huo unatarajiwa kufikia maafikiano zaidi kuhusu ushirikiano wa kiuchumi.

"Ninatarajia mkutano huo utatoa urahisi zaidi kwa mabadilishano ya watu kati ya Kyrgyzstan na China," amesema, huku akiongeza kuwa mabadilishano baina ya watu yanaweza kuongeza hisia na maelewano kati ya watu wa nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wake, mkutano huo utatoa jukwaa jipya kwa nchi za Asia ya Kati ili kuimarisha ushirikiano wao na China na kuendeleza zaidi ushirikiano chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha