Mradi mkubwa zaidi wa usambazaji maji katika Jimbo la Malanje, Angola wakabidhiwa rasmi

(CRI Online) Mei 15, 2023

Hafla ya kukabidhiwa kwa mradi mkubwa zaidi wa uimarishaji wa mfumo wa usambazaji maji katika Jimbo la Malanje, Angola, uliotekelezwa na Kampuni ya China Petroleum Pipeline Engineering, imefanyika Tarehe 12. Rais wa Angola Bw. João Lourenço alihudhuria hafla hiyo na kukata utepe.

Bw. Lourenço alisema kuwa maji safi ya kunywa yanayotolewa na mfumo huo yanaweza kuzuia kuenea kwa magonjwa, kulinda ipasavyo afya za watu wa eneo hilo, na kuchangia kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kampuni ya China, mradi huo ni kituo cha kwanza cha usambazaji maji kwa saa 24 katika eneo hilo, ambacho kimeongeza wigo wa mradi wa usambazaji wa maji kwa takriban mara 6 na kunufaisha zaidi ya wenyeji 330,000.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha