Watu 33 wauawa katika shambulizi la kigaidi nchini Burkina Faso

(CRI Online) Mei 15, 2023

Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa watu wasiopungua 33 wameuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea katika eneo la Boucle du Mouhoun, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Gavana wa Mouhoun ambako eneo hilo la Boucle du Mouhoun linapatikana amesema Kijiji cha Youlou kilikumbwa na shambulizi la kikatili, ambapo watu wenye silaha walishambulia raia wanaojishughulisha na mambo ya kilimo cha mboga kwenye ukingo wa mto, na kusababisha vifo vya watu.

Tangu Mwaka 2015, hali ya ukosefu wa usalama katika nchi hiyo imesababisha vifo vya watu wengi na maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha