Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Disketi ya USB ya kumbukumbu za Reli ya Mombasa-Nairobi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2023

Picha ikionehsa disketi ya USB ya kumbukumbu za Reli ya Mombasa-Nairobi ambayo ni zawadi aliyotoa Rais wa Kenya wa wakati huo Uhuru Kenyatta kwa Rais Xi Jinping mwezi Mei, 2017. (Picha/Hu Yang)

Picha ikionehsa disketi ya USB ya kumbukumbu za Reli ya Mombasa-Nairobi ambayo ni zawadi aliyotoa Rais wa Kenya wa wakati huo Uhuru Kenyatta kwa Rais Xi Jinping mwezi Mei, 2017. (Picha/Hu Yang)

Tarehe 14, Mei, 2017 Rais wa Kenya wa wakati huo Uhuru Kenyatta aliwasili China kuhudhuria kwenye mkutano wa kwanza wa viongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Alipohojiwa kabla ya kufunga safari ya kuja China, kwa mahususi aliishukuru China kwa sababu ya Reli ya Mombasa-Nairobi, ambayo ilikuwa karibu kuzinduliwa baada ya kujengwa kwa msaada wa kampuni ya China. Kenyatta aliweka shukurani zake kwenye disketi ya USB yenye vifundo vya mapambo mekundu ya Kichina. Hii ni zawadi aliyoandaa kwa ajili ya Rais Xi Jinping wa China.

Kwenye upande wa mbele wa disekti hiyo, kuna maneno ya “Reli ya Mombasa-Nairobi”. Video inayoonesha Reli ya Mombasa-Nairobi na mandhari ya mazingira asili ya Kenya imehifadhiwa ndani ya disketi hiyo. Kwenye video hiyo, wajenzi wa reli hiyo wa China na Kenya wanaonekana wakitabasamu bega kwa bega.

Xi alipokutana na Kenyatta alisema, ujenzi wa reli ya Mombasa-Nairobi inabidi utumike kama mwanzo wa kusukuma mbele ujenzi wa ukanda wa kiuchumi wa viwanda unaounganisha bandari na reli, na alipendekeza kupandisha hadhi ya uhusiano kati ya China na Kenya kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

Takwimu zinaonesha kuwa, hadi nusu ya kwanza ya mwaka 2022, kwa jumla reli ya Mombasa-Nairobi ilisafirisha abiria milioni 7.94, makontena za milioni 1.82, na mizigo yenye uzito wa tani milioni 20.29.

Tarehe 15, Mei, 2017, Rais Xi Jinping wa China alikutana na Rais wa Kenya wa wakati huo Uhuru Kenyatta ambaye aliwasili China kuhudhuria kwenye mkutano wa kwanza wa viongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa  “Ukanda Mmoja, Njia Moja” hapa Beijing.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha