Kampuni za Tanzania zajipanga kushiriki katika Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2023

Picha hii iliyopigwa Mei 15, 2023 ikionyesha kongamano la Tanzania la kutangaza na kuhamasisha Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China jijini Dar es Salaam, Tanzania. Viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara nchini Tanzania Jumatatu walisema wanatarajia kutafuta zaidi soko la China kwa kushiriki katika Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yatakayofanyika Shanghai Mwezi Novemba. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

DAR ES SALAAM - Viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara nchini Tanzania Jumatatu walisema wanatarajia kutafuta zaidi soko la China kwa kushiriki katika Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yatakayofanyika Shanghai Mwezi Novemba.

Tangazo hilo limetolewa na maofisa waandamizi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Shirikisho la Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Zanzibar (ZNCC).

Akizungumza kwenye kongamano la utangazaji na uhamasishaji lililoandaliwa na Ofisi ya Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China na ubalozi wa China nchini Tanzania, Meneja wa Fedha wa TPSF, Deogratius Massawe amesema shirika lake litahamasisha sekta binafsi ya Tanzania kushiriki katika maonyesho hayo.

Naye mwakilishi kutoka TCCIA, Nebart Mwapwele amesema shirika hilo limejipanga kuhamasisha wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki katika maonyesho hayo ambayo yataleta fursa kwa bidhaa za Tanzania kuingia katika soko la China na masoko katika nchi nyingine za Bara la Asia.

“Pia itaimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Tanzania,” Mwapwele amesema.

Suo Peng, Konsela wa ubalozi wa China nchini Tanzania, amesema maonyesho hayo ni jukwaa bora kwa watumiaji wa China kujua "Made in Tanzania (Vinavyotengenezwa nchini Tanzania)" na kupenda bidhaa za Tanzania.

"Tunatumai kuwa bidhaa na huduma za Tanzania zinaweza kuingia maono ya watumiaji wa China kupitia dirisha la CIIE, kusimama kidete na faida zake yenyewe, na kuanzisha uhusiano wa karibu wa ushirikiano na wabia wa China," Suo amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha