Mwanafunzi wa Turkmenistan nchini China: Mimi ni shuhuda wa urafiki kati ya China na nchi za Asia ya Kati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2023

Bayram Durdyyev Rahman, mwanafunzi wa Turkmenistan anayesoma nchini China. (Picha imepigwa na Zhang Wenjie/People’s Daily Online)

Bayram Durdyyev Rahman, mwanafunzi wa Turkmenistan anayesoma nchini China. (Picha imepigwa na Zhang Wenjie/People’s Daily Online)

“Nyinyi ni mashuhuda, wanufaika, wajenzi na wawasilishaji wa uhusiano kati ya China na nchi za Asia ya Kati. Ninatumai mtashiriki kikamilifu katika lengo la kujenga urafiki kati ya China na nchi za Asia ya Kati, kuendeleza moyo wa ‘Njia ya Hariri’, kusimulia vizuri simulizi za China na Asia ya Kati, na kuwa wajumbe wazuri wa urafiki na daraja la ushirikiano……” Tarehe 15, habari kwamba Rais Xi Jinping wa China alijibu barua ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Petroli cha China (Beijing) wanaotoka nchi za Asia ya Kati iliyokuwa na nukuu hiyo iliwafanya wanafunzi hao kuwa na furaha kubwa.

Alipopata habari hiyo, mwanafunzi wa kigeni kutoka Turkmenistan Bayram Durdyyev Rahman hakuweza kuficha furaha yake kubwa, “Tulikuwa tunatarajia kitu fulani tulipomwandikia barua Rais Xi Jinping, lakini kamwe hatukutarajia kupokea majibu yake ya barua.”

Rahman amesema, alikuja China kusoma chuoni chini ya msaada wa Programu ya Udahili wa pamoja wa Wanafunzi wa China na Turkmenistan. Kama alivyoandika Rais Xi katika barua yake ya majibu, “mimi ni mnufaika wa urafiki kati ya China na nchi za Asia ya Kati.”

Rahman akijisomea kwenye chumba cha kujisomea. (Picha imepigwa na Zhang Wenjie/People’s Daily Online)

Rahman akijisomea kwenye chumba cha kujisomea. (Picha imepigwa na Zhang Wenjie/People’s Daily Online)

Ili kubeba wajibu wa kijamii, tangu Mwaka 2009, Kampuni ya Mto Amu Darya Turkmenistan ya Shirika la Kitaifa la Petroli la China pamoja na Chuo Kikuu cha Petroli cha China zilianzisha programu ya kuteua wahitimu bora wa sekondari wa Turkmenistan kwenda kwenye chuo hicho kwa ajili ya kusoma. Mnamo Mwaka 2010, Rahman aliteuliwa kwenda kusoma China kupitia programu hiyo.

Baada ya kufika China, alianza kujifunza lugha ya Kichina. Katika miaka iliyofuata alihitimu masomo ya kujiandaa ya lugha ya Kichina, shahada ya kwanza ya Uhandisi wa Kikemia, shahada ya uzamili ya Usimamizi…… katika safari yake ya masomo, Rahman amekuwa akiishi China kwa miaka 13, na amekuwa “mwenye uzoefu” kwa wanafunzi wapya.

Alipokuwa akitembea kwenye kampasi ya chuo, alikuwa akikutana na kusalimiana mara kwa mara na watu wanaomfahamu. “Wanafunzi wa kigeni hapa karibu wote wananifahamu” alisema. Hata hivyo, alipokuja China alikuwa na “wasiwasi wa kijamii” kiasi. "Wakati wa utoto nilikuwa mwenye haya, na ilikuwa ni changamoto kubwa kwangu kuzoea mazingira mapya.”

Chini ya uangalizi na msaada wa walimu wake na wanafunzi wenzake, Rahman alianza kujibadilisha, na kuendana na mazingira mapya hatua kwa hatua.

Rahman ana hamasa sana kuhusu kazi ya kuwahudumia wanafunzi, hali ambayo pengine inatokana na hili. Anasema: “kwa kuwa ninajua kabisa changamoto gani nilikabiliana nazo wakati wa kuingia mazingira mapya, natumai wengine wanaweza kukwepa hayo chini ya msaada wangu.”

Mnamo mwaka 2020, janga la ghafla la virusi vya Korona lilivuruga ratiba yake ya maisha na masomo. Rahman alirudi nyumbani kwao kwa muda, lakini siku zote moyoni mwake alikuwa akikumbuka chuo chake. Mwaka huu hatimaye Rahman ameweza kurudi tena kwenye chuo chake. Hivi sasa msimu wa kuhitimu unawadia, na ameanza kufanya maandalizi kwa ajili ya kutetea tasnifu yake ya shahada ya uzamivu. Tasnifu yake ya shahada ya uzamivu ni kuhusu “Kuufanya Umarksi kuwa wa Kichina". Chaguo hili la tasnifu huwashangaza wenzake, ambao wanadhani kuwa utaaluma wake umebadilika sana.

Lakini Rahman ameeleza kuwa, “masuala mengi yaliyoibuliwa na Marx na Engels bado yana uhalisia na yenye ufanisi katika jamii ya sasa. Maendeleo ya haraka ya China yanaonekana kwa kila mtu. Kuufanya Umarksi kuwa wa Kichina kunastahili kuchambuliwa na kupata somo. Kupitia kufanya utafiti tunaweza kuelewa njia ya maendeleo ya China. Si lazima nchi nyingine ziiige kabisa, lakini tunaweza kuchukua maendeleo ya China kama mfano.”

Turkmenistan ilikuwa kituo muhimu katika “Njia ya Hariri” ya kale, ambayo kupitia kwake bidhaa kutoka China zinaendelea kusafirishwa kwenda Ulaya. Leo pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limemfanya Rahman aone mabadiliko halisi ambayo limeleta kwa watu wa Turkmenistan na China. “Katika miaka ya hivi karibuni, thamani ya biashara kati ya China na Turkmenistan imekuwa ikipanda juu, na kampuni nyingi za uchukuzi za Turkmenistan zinataka kufanya biashara na China. Kutoka simu ndogo za mkononi, kompyuta hadi mashine kubwa za kuchakata mafuta viwandani. Bidhaa nyingi katika maisha yetu zinatengenezwa na kampuni za China” amesema.

Katika majira ya joto ya mwaka huu, Rahman atahitimu kutoka chuo. “Nimeishi hapa kwa miaka 13 na ninakipenda chuo changu kutoka chini ya moyo. Ingawa bado sijaondoka, tayari nimeshaanza kukikumbuka.”

Rahman amesema, bila kujali atakuwepo wapi siku za mbele, “Barua ya majibu ya Rais Xi itakuwa jambo kubwa zaidi lisiloweza kusahaulika na kumbukumbu yenye thamani zaidi katika muda wangu wa kuishi China,.” Anatumai atatoa mchango kwa ushirikiano kati ya China na nchi za Asia ya Kati kwa kupitia juhudi zake mwenyewe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha