Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 18, 2023

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, ambaye yuko China  kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa China na Nchi za Asia ya Kati na kufanya ziara ya kiserikali, mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 17, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

Rais wa China Xi Jinping Jumatano alifanya mazungumzo mjini Xi'an na Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, ambaye yuko China kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Viongozi wakuu wa China na Nchi za Asia ya Kati na kufanya ziara ya kiserikali.

Rais Xi amemkaribisha Tokayev kwa furaha kuja China kuhudhuria kwenye mkutano huo wa viongozi wakuu na kufanya ziara ya kiserikali. Ameelezea furaha yake kwa kukutana na Tokayev huko Xi'an na pia kumtakia furaha ya siku ya kuzaliwa ambapo siku hiyo alikuwa akitimiza miaka 70 tangu kuzaliwa kwake.

Rais Xi amesema kuwa ziara ya kiserikali ya Tokayev nchini China katika mazingira hayo maalum inathibitisha kwa kiwango kikubwa juu ya nguvu ya uhusiano wa pande hizo mbili na kwa mara nyingine inathibitisha uhusiano wake wa kipekee na China.

“Pande hizi mbili zinapaswa kuendeleza kwa dhati urafiki wa jadi, kusaidiana kithabiti, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, kutafuta maendeleo na ustawishaji, na kujenga jumuiya ya China na Kazakhstan yenye mustakabali wa pamoja, na kuwa na urafiki wa kudumu, kuaminiana na kushikamana ” Rais Xi amesema.

Ameeleza kuwa China na Kazakhstan zimefanikiwa kutekeleza miradi kadhaa muhimu ya ushirikiano tangu alipotoa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja miaka 10 iliyopita.

Huku akikaribisha uanzishaji wa mwaka wa utalii wa Kazakhstan nchini China Mwaka 2024, Rais Xi ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za kupanua ushirikiano katika uchumi, biashara, uwekezaji, kilimo, uundaji wa magari na nishati, kuimarisha mafungamano ya mawasiliano, na kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na biashara ya mtandaoni, uvumbuzi na data kubwa.

Amesema mkutano wa viongozi wakuu ni wenye umuhimu mkubwa na utaingiza ushirikiano kati ya China na Asia ya Kati katika zama mpya.

Rais Tokayev amesema kuwa, anakubaliana kabisa na Rais Xi juu ya tathmini ya uhusiano wa pande mbili na mapendekezo ya kuimarisha ushirikiano zaidi. Huku akisisitiza nafasi maalum na muhimu ya China katika sera ya mambo ya nje ya nchi yake, amesema uhusiano kati ya Kazakhstan na China umejengwa juu ya urafiki imara na kuaminiana kwa pande zote na kufurahia malengo na dhamira ya pamoja.

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, ambaye yuko China kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa China na Nchi za Asia ya Kati na kufanya ziara ya kiserikali, mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 17, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, ambaye yuko China kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa China na Nchi za Asia ya Kati na kufanya ziara ya kiserikali, mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 17, 2023. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha