Mkoa wa Xinjiang wa China wajenga vituo 39,000 vya msingi vya Teknolojia ya 5G

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 18, 2023
Mkoa wa Xinjiang wa China wajenga vituo 39,000 vya msingi vya Teknolojia ya 5G
Picha hii kutoka kwenye kumbukumbu isiyo na tarehe ikionyesha mfanyakazi akisakinisha vifaa kwenye kituo cha msingi cha teknolojia ya 5G katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China. (Xinhua)

URUMQI - Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China ulikuwa umejenga vituo 39,000 vya msingi vya teknolojia ya 5G kufikia mwishoni mwa Aprili 2023, huku ukiweka juhudi za kusukuma mbele mitandao ya 5G, serikali ya mkoa huo imesema Jumatano.

Hivi sasa, miji yote ya ngazi ya chini ya mkoa huo, maeneo yote na asilimia 99.16 ya vitongoji vyake vimefikiwa na mitandao ya 5G. Kuna vituo 15 vya msingi vya teknolojia ya 5G kwa kila wakazi 10,000 katika Mkoa wa Xinjiang.

Ma Zhuqing, Mkuu wa Idara ya mawasiliano ya mkoa huo amesema kuwa, mwaka jana, sekta ya habari na mawasiliano ya Xinjiang iliwekeza yuan bilioni 1.7 (kama dola milioni 244 za Kimarekani) katika kujenga vituo vya msingi vya teknolojia ya 5G.

Xinjiang pia inaharakisha uunganishaji na uvumbuzi wa programu zake muhimu za kiviwanda za teknolojia ya 5G, huku programu 70 muhimu za teknolojia ya 5G katika viwanda husika zikiendelea, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bandari ya nchi kavu inayotumia teknolojia za akili bandia katika kituo cha ukusanyaji bidhaa cha treni za mizigo za China na Ulaya (Urumqi).

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha