Ripoti ya Umoja wa Mataifa yainua makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China

(CRI Online) Mei 18, 2023

Ripoti iliyotolewa juzi na Umoja wa Mataifa kuhusu Hali na Matarajio ya Uchumi wa Dunia Katikati ya Mwaka 2023 iliinua makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kutoka asilimia 4.8 hadi asilimia 5.3, na mashirika ya kimatiafa yakiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) hivi karibuni pia yaliinua makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka huu. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alisema, hii inaonesha imani ya jumuiya ya kimataifa kwa mustakabali wa uchumi wa China.

Bw. Wang ameeleza imani yake kuwa China itaendelea kutia mkazo na nguvu kwa ajili ya kufufuka kwa uchumi wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha