Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa UN akaribisha uamuzi wa Russia wa kuongeza muda wa mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuongeza muda wa Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 17, 2023. (Xinhua/Xie E)
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatano alikaribisha uamuzi wa Russia ambao utaruhusu kuongezwa kwa muda wa Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi, ambao unaruhusu mauzo ya nafaka na mazao mengine ya kilimo ya Ukraine kutoka bandari za Bahari Nyeusi.
"Tuna kiasi fulani cha maendeleo mazuri na muhimu: uthibitisho wa Shirikisho la Russia kuendeleza ushiriki wake katika Mpango wa Bahari Nyeusi kwa siku nyingine 60. Ninakaribisha uamuzi huu," amesema Guterres. "Mwendelezo huu ni habari njema kwa Dunia."
Masuala muhimu bado yanabaki bila kutatuliwa, lakini wajumbe wa Russia, Ukraine, Uturuki na Umoja wa Mataifa wataendelea kuyajadili, amewaambia waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. "Natumai tutafikia makubaliano ya kina ili kuboresha, kupanua na kuongeza muda wa mpango huo, kama nilivyopendekeza katika barua ya hivi majuzi kwa marais wa nchi hizo tatu."
Amesema, chini ya Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi, zaidi ya tani milioni 30 za chakula zimeuzwa nje ya nchi. Vyakula muhimu vinavyosambazwa vinawafikia baadhi ya watu na maeneo yaliyo hatarini zaidi duniani, ikiwa ni pamoja na tani 30,000 za ngano ambazo zimetoka majuzi tu Ukraine kulisha watu wenye njaa nchini Sudan.
Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi ulitiwa saini katika maeneo tofauti na Russia na Ukraine huko Istanbul pamoja na Uturuki na Umoja wa Mataifa mnamo Julai 22, 2022. Mkataba huo, ambao ulianza kutumika kwa siku 120, uliongezwa muda wake katikati ya Novemba 2022 kwa siku 120 hadi Machi 18, 2023. Wakati huo, Russia ilikubali tu kuongeza mkataba huo kwa siku 60 zaidi, hadi Mei 18, 2023.
Kama sehemu ya makubaliano ya sambamba ya mpango huo wa nafaka, Russia na Umoja wa Mataifa zilitia saini mkataba wa makubaliano juu ya kuwezesha mauzo ya nje ya chakula na mbolea ya Russia. Lakini makubaliano hayo ya sambamba hayajapata maendeleo makubwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuongeza muda wa Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 17, 2023. (Xinhua/Xie E)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuongeza muda wa Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 17, 2023. (Xinhua/Xie E)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma