Rais Samia Suluhu Hassan asema Tanzania inatafakari kuhusu kurusha satelaiti yake kwenye anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2023

DAR ES SALAAM - Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Alhamisi ameweka wazi kuwa mipango ilikuwa inaendelea kurusha satelaiti ya taifa hilo kwenye anga ya juu.

Tanzania itaungana na nchi jirani za Kenya na Uganda ambazo zimeunda na kurusha satelaiti kwenye anga ya juu katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Akizindua Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Habari ya Azam, ambayo ni kampuni kubwa ya kibinafsi ya habari nchini jijini Dar es Salaam, Tanzania, Rais Samia amesema mazungumzo ya kurusha satelaiti hiyo kwenye anga ya juu yameanza.

Kwa mujibu wa ripoti zilizopo, Mwezi Aprili mwaka huu Kenya ilituma kwenye anga ya juu satelaiti yake ya kwanza ya uchunguzi iliyobebwa na roketi ya SpaceX kutoka Marekani, ambayo ina uwezo wa kukusanya data za kilimo na mazingira, ikiwa ni pamoja na mafuriko ya maji, ukame na moto wa nyikani, ambazo serikali inapanga kuzitumia kukabiliana na majanga na kutokomeza hali ya ukosefu wa usalama wa chakula.

Uganda ilirusha satelaiti yake ya kwanza kabisa katika kituo cha anga ya juu cha kimataifa mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha