

Lugha Nyingine
Jeshi la Sudan lasema litafanya juhudi kutimiza makubaliano ya kusimamisha vita
(CRI Online) Mei 22, 2023
Jeshi la Sudan limetangaza ahadi yake kwa makubaliano ya muda mfupi ya kusimamisha vita na mpangilio wa kibinadamu yaliyosainiwa kati yake na kikosi cha RSF huko Jeddah, Saudi Arabia.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la Sudan imesema, jeshi hilo limeahidi kutimiza makubaliano hayo na linatumai kikosi cha RSF nacho kitafanya hivyo.
Taarifa hiyo pia imesema, muda wa kusimamisha vita ni siku saba na utatekelezwa kuanzia saa nne kasorobo usiku wa Jumatatu kwa saa za huko.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, pande mbalimbali zitatekeleza kwa pande zote makubaliano hayo na kuhakikisha kuwa vikosi vyote chini ya uongozi na udhibiti wao vitafuata makubaliano hayo kwa muda wote na kwa kikamilifu.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma