Rais wa Angola asifu kituo cha umeme kilichojengwa na China kwa mchango wake katika uchumi na jamii

(CRI Online) Mei 22, 2023

Rais wa Angola Joao Laurenco amesifu mchango wa kijamii na kiuchumi unaotolewa na kituo cha umeme cha Caculo-Cabaca kilichojengwa na China, akisema kitaleta manufaa dhahiri katika upatikanaji wa umeme na kuboresha maisha ya Waangola.

Rais Lourenco amesema hayo jumamosi katika hafla ya kuzindua njia ya mchepuko ya muda ya Mto Cuanza, ambayo inaashiria kuanza kwa awamu kuu ya ujenzi wa mradi huo wa umeme, ambao utakuwa mkubwa zaidi nchini Angola na wa tatu kama huo kukamilika barani Afrika.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Maji wa Angola Joao Baptista Borges amesifu uhusiano kati ya Angola na China katika kuboresha matumizi ya nishati safi nchini Angola.

Hivi sasa mradi huo umetoa ajira kwa zaidi ya wafanyakazi 2,500, ambao zaidi ya asilimia 81 ni wakazi wa eneo ambalo mradi huo unatekelezwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha