Watafiti wataka juhudi zaidi zitumike kuwalinda mbwa mwitu wa Ethiopia walio hatarini

(CRI Online) Mei 22, 2023

Chuo Kikuu cha Kiebrania cha mjini Yerusalem kimesema, utafiti umethibitisha uwepo wa mbwa mwitu wa Ethiopia miaka milioni 1.5 iliyopita.

Katika utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Nature Communications Biology, watafiti kutoka Chuo Kikuu hicho wakishirikiana na wenzao kutoka Hispania, Marekani, Italia na Ethiopia, walitafiti kwa pamoja mabaki ya fuvu la chini la mbwa mwitu wa Ethiopia lililogunduliwa mwaka 2017 katika eneo la Melka Wakena.

Kwa mujibu wa utafiti huo, mabaki hayo ni ya miaka milioni 1.5 iliyopita, matokeo yanayokinzana na madai ya awali kuwa mbwa mwitu wa Ethiopia walikwenda Afrika wakitokea nchi za Ulaya na Asia miaka karibu 20,000 iliyopita.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha