Vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika vyaahidi kuimarisha operesheni dhidi ya Al-Shabaab huko Jowhar

(CRI Online) Mei 22, 2023

Maofisa waandamizi wa polisi na jeshi wa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) wamekutana na maofisa wa polisi wa Jimbo la Hirshabelle na kuahidi kuimarisha mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab kwenye eneo la Jowhar, kati na kusini mwa Somalia.

Kamanda wa kikosi cha Burundi cha ATMIS Jean Claude Niyiburana, ambaye aliongoza mkutano huo wa Jumamosi kujadili njia za kuhimiza ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab kwenye eneo la Jowhar, amesema wamekuwa na mawasiliano na majadiliano mazuri kuhusu namna ya kufanya kazi kwa pamoja na kupanga mashambulizi yenye ufanisi dhidi ya magaidi wa Al-Shabaab.

Kwa mujibu wa ATMIS, tume hiyo imeongeza kasi ya maandalizi ya kuondoa askari elfu mbili kutoka nchini Somalia kabla ya Juni 30 mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha