Safari inayofuata ya chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou XVI kuanza hivi karibuni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 23, 2023

http://img2.chinadaily.com.cn/images/202305/22/646b3ec8a310b60580cd6ac9.jpeg

Picha iliyopigwa Mei 22, 2023 ikionyesha chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou XVI na roketi ya kubeba ya Long March 2F Y16 vikihamishwa hadi eneo la urushaji katika Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan kwenye Jangwa la Gobi, Kaskazini-Magharibi mwa China. [Picha na Wang Jiangbo/Chinadaily]

Safari inayofuata ya chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou XVI, imepangwa kufanyika katika siku zijazo ili kuwasafirisha wanaanga watatu hadi kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong, kwa mujibu wa mipango iliyofanywa na Shirika la Anga ya Juu la China.

Chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou XVI na roketi yake ya kubeba ya Long March 2F, tayari vimehamishwa kwenye mnara wa huduma siku ya Jumatatu kwenye Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan kilichoko Jangwa la Gobi, Kaskazini Magharibi mwa China, shirika hilo limesema katika taarifa fupi kwa vyombo vya habari, na kuongeza kuwa chombo hicho na roketi hiyo vitafanyiwa ukaguzi wa mwisho katika siku kadhaa zijazo.

Shenzhou XVI itakuwa safari ya kwanza ya wanaanga kutembelea Tiangong mwaka huu na ya kwanza kuwasili tangu ujenzi wake ukamilishwe na wanaanga walioruka na Vyombo vya Shenzhou XIV na XV.

http://img2.chinadaily.com.cn/images/202305/22/646b3ec8a310b60580cd6acc.jpeg

Picha iliyopigwa Mei 22, 2023 ikionyesha chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou XVI na roketi ya kubeba ya Long March 2F Y16 vikihamishwa hadi eneo la urushaji katika Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan kwenye Jangwa la Gobi, Kaskazini-Magharibi mwa China. [Picha na Wang Jiangbo/Chinadaily]

Wanaanga hao watakaosafiri na chombo hicho, ambao majina yao bado hayajawekwa wazi, watachukua kituo kikubwa cha obiti kutoka kwa timu ya wanaanga waliosafiri na Chombo cha Shenzhou XV, ambao ni mkuu ujumbe Meja Jenerali Fei Junlong, Kanali Mwandamizi Deng Qingming na Kanali Mwandamizi Zhang Lu, ambao waliwasili Novemba 30 mwaka jana. Hadi kufikia mwishoni mwa Mei, wanaanga hawa chini ya uongozi wa Fei watakuwa wamekaa kwenye obiti kwa miezi sita.

Mapema mwezi huu, chombo cha anga ya juu cha kubeba mizigo cha roboti cha Tianzhou 6 kiliruka kutoka katika Kituo cha Urushaji vyombo kwenye Anga ya Juu cha Wenchang katika Mkoa wa Hainan ili kusafirisha vifaa kwa ajili ya safari inayofuata ya wanaanga, na kuwa chombo cha kwanza cha anga ya juu kuzuru kituo cha anga ya juu cha Tiangong mwaka huu.http://img2.chinadaily.com.cn/images/202305/22/646b3ec8a310b60580cd6acf.jpeg

Picha iliyopigwa Mei 22, 2023 ikionyesha chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou XVI na roketi ya kubeba ya Long March 2F Y16 vikihamishwa hadi eneo la urushaji katika Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan kwenye Jangwa la Gobi, Kaskazini-Magharibi mwa China. [Picha na Wang Jiangbo/Chinadaily]

http://img2.chinadaily.com.cn/images/202305/22/646b3ec8a310b60580cd6ad2.jpeg

Picha iliyopigwa Mei 22, 2023 ikionyesha chombo cha anga ya juu cha China, Shenzhou XVI na roketi ya kubeba ya Long March 2F Y16 vikihamishwa hadi eneo la urushaji katika Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan kwenye Jangwa la Gobi, Kaskazini-Magharibi mwa China. [Picha na Wang Jiangbo/Chinadaily]

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha