Nini imetokea kuhusu kahawa tangu iingizwe China?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 23, 2023

Miaka zaidi ya 100 imepita tangu mbegu ya kwanza ya mbuni ilipopandwa nchini China, lakini katika miaka 20 hadi 30 ya hivi karibuni iliyopita, ndipo biashara ya kahawa ya China ilipoanza kupata maendeleo ya kasi. Katika miaka ya hivi karibuni, soko la kahawa la China kila mwaka limepata ongezako la asilimia 20 hivi, ambayo imezidi kwa kiasi kikubwa asilimia 2 ya dunia. Taasisi husika inakadiri kuwa, thamani ya shughuli za kahawa nchini China itazidi Yuan trilioni moja ifikapo mwaka 2025, hali ambayo inaonesha uwezo mkubwa wa soko la kahawa la China.

Jiografia ya kahawa ya China

Kijiji cha Zhukula cha Mkoa wa Yunnan, China ni sehemu ambako mibuni ilipandwa kwanza katika China, ambapo Wachina walipata kuonja kwa mara ya kwanza kahawa ya kienyeji ya huko. Mnamo mwaka 1892, mmisionari wa Kikatoliki wa Ufaransa aliyekuja kijiji hicho, alipanda mibuni kwenye eneo dogo huko, na kuwafundisha wanakijiji wa huko namna ya kupanda mibuni, kusaga buni na kutengeneza kahawa. Kinywaji hicho kipya kilivutia wanakijiji wa huko. Hadi hivi sasa, wanakijiji wa kabila la Wa-yi wa kijiji hicho bado wana desturi ya kunywa kahawa.

Lakini katika kahawa ya Yunnan tunayokunywa hivi sasa, ni kiasi kidogo tu kinatokana na aina ya mibuni ya Kijiji cha Zhukula. Mwaka 1914, watu wa Kabila la Wa-Jingpo wanaoishi kwenye mipaka ya China waliingiza na kupanda mibuni huko Ruili ya Yunnan kama miti ya mapambo uani. Baadaye mwaka 1952, watafiti wa Taasisi ya Sayansi ya Kilimo ya Yunnan waligundua miti hiyo ya kahawa, na ikawa imechukuliwa kama aina kuu ya mibuni ya kahawa inayostawishwa zaidi mkoani Yunnan.

Sambamba na kuanzishwa kwa kituo cha biashara ya kahawa cha Yunnan na cha Chongqing, serikali ya mikoa na wahusika wa biashara hiyo ya China pia wanawasaidia wakulima wa kahawa kuongeza sifa ya upandaji wa mibuni, na shughuli za upandaji wa mibuni zimeendelezwa vizuri siku hadi siku nchini China.

Maendeleo ya kahawa katika China

Kuanzia mwisho wa Enzi ya Qing ya China (B.K. 1636-1912) hadi zama za Jamhuri ya China (B.K.1921-1949), sehemu kadhaa za China zilifungua mlango wao kwa nchi za nje, na biashara kati ya China na nchi za magharibi zilikuwa nyingi. Shughuli za Kahawa zilipata maendeleo katika miji ya Shanghai, Nanjing na Guangzhou.

Ilipofika miaka ya 1980, sera ya mageuzi na kufungua mlango ilitekelezwa kwa hali moto moto nchini China, ambapo Wachina wengi walikwenda kufanya kazi katika miji ya Kusini-Mashariki na eneo la pwanipwani la Mashariki, na kahawa ya haraka ikiwa kinywaji cha kuchangamsha na kuongeza nguvu ilipendwa sana na watu.

Baada ya kuingia karne ya 21, maendeleo ya miji na ya ujenzi wa mambo ya kisasa yameanza kupatikana nchini China, ambapo kahawa freshi iliyochemshwa ilianza kupendwa na watu kutokana na kuingia kwa Starbucks na chapa nyingine za kahawa. Kahawa ilikuwa imepewa sifa ya kufurahisha na kupata raha.

Katika muda wa karibu miaka 10 iliyopita, bidhaa za kahawa zinaelekea kuwa kahawa yenye ubora zaidi, na kahawa ya kupikwa kwa mkono ndiyo alama moja ya maendeleo yake. Mikahawa midogomidogo iliyojengwa vizuri na kuwavutia watu imejitokeza na kukua mitaani popote. Mwaka 2017, Starbucks ilianzisha kiwanda chake cha pili duniani cha kukaanga buni kiitwacho “Uteuzi Bora” huko Shanghai.

Licha ya hayo, kutokana na maendeleo kasi ya miji, mtindo wa maisha ya kasi, pamoja na ustawi wa sekta ya huduma, mahitaji ya watu mijini yanaongezeka zaidi, na shughuli za kutengeneza kahawa zenye sifa ya bei nafuu na urahisi zimepata uwekezaji zaidi na kupanua siku hadi siku, ambapo idadi ya mikahawa ya Shanghai iliyotia fora duniani ndiyo iliyoonesha maendeleo ya kipindi hiki.

Kahawa za kuchanganya za China

Kahawa ya dawa ya mitishamba ya jadi ya Kichina, kahawa iliyotengenezwa kwa pombe... kahawa yenye uvumbuzi na ya kuvutia kwa mara nyingi huwa bidhaa moto moto zaidi hapa China.

Katika Eneo la Teknolojia ya Juu la Mji wa Xi'an, Mkoa wa Shaanxi Kuna kijiwe cha kahawa cha ujasiriamali kikiwa na vifaa vya kahawa na utamaduni wa kahawa kama maudhui yake. Maduka ya kahawa katika kijiwe hicho hutoa saluni za ujasiriamali, mafunzo ya kuandaa wajasiriamali, madarasa, vitabu vya kusoma, na kadhalika.

Mtindo wa uuzaji wa kahawa umeunganishwa na uchumi wa kidijitali na biashara ya uchukuzi wa bidhaa iliyostawi ya China, na pia unapanuka kila wakati, kama vile uuzaji kahawa papo hapo, roboti za kahawa, mashine otomatiki za kahawa, kahawa ya O2O, na kadhalika hutoa kahawa safi kila wakati kwa kila tukio maishani.

Soko la kahawa linaloshamiri nchini China pia limevutia kampuni nyingi ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na kahawa kujiunga nalo, kama vile kahawa maarufu ya hivi karibuni ya China Post, Gloria Coffee chini ya Tianjin Goubuli Baozi, EasyJet Coffee chini ya Sinopec, na kadhalika.

Uuzaji wa kahawa za kuchanganya umekuwa mtindo mpya katika soko la kahawa la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha