

Lugha Nyingine
Kazi ya pamoja kati ya China na Indonesia ya uthibitishaji ubora na majaribio ya Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung yaanza
Picha hii ya angani iliyopigwa Tarehe 22 Mei 2023 ikionyesha treni ya ukaguzi wa kina ikiendeshwa kwenye Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung nchini Indonesia. (Picha na Kampuni ya Kimataifa ya Reli ya China /Xinhua)
Wafanyakazi na waandishi wa habari wakiwa wanapanda treni ya ukaguzi wa kina wakati wa kazi ya pamoja ya uthibitishaji ubora na majaribio ya Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung nchini Indonesia, Mei 22, 2023. (Picha na Ren Weiyun/Xinhua)
Wahandisi wakifanya majaribio ya umeme kwenye treni ya ukaguzi wa kina wakati wa kazi ya pamoja ya uthibitishaji ubora na majaribio ya Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung nchini Indonesia, Mei 22, 2023. (Picha na Ren Weiyun/Xinhua)
Picha hii ya angani iliyopigwa Tarehe 22 Mei 2023 ikionyesha treni ya ukaguzi wa kina ikiendeshwa kwenye Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung nchini Indonesia. (Picha na Kampuni ya Kimataifa ya Reli ya China /Xinhua)
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha madereva wa treni ya mwendokasi ya EMU wakiendesha treni ya ukaguzi wa kina kwenye Reli ya Mwendokasi Kasi ya Jakarta-Bandung nchini Indonesia, Mei 22, 2023. (Xinhua/Xu Qin)
JAKARTA - Kazi ya pamoja kati ya China na Indonesia ya uthibitishaji ubora na majaribio ya Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung (HSR) imeanza Jumatatu, na kuashiria hatua muhimu katika ujenzi wa mradi wa reli hiyo.
Uthibitishaji ubora na majaribio hayo ya pamoja yanafanywa kabla ya kuzinduliwa na kuanza kufanya kazi rasmi kwa reli hiyo ya mwendo kasi ili kuhakikisha uendeshaji salama na mzuri wa treni.
Kwa kufanya majaribio hayo ya kivitendo kwa kutumia treni ya ukaguzi wa kina kwenye reli hiyo mpya ya mwendo kasi iliyojengwa, utendakazi wa mifumo mbalimbali kama vile reli, usambazaji wa umeme, mfumo wa juu zaidi, mawasiliano, utoaji wa ishara na ufuatiliaji wa tahadhari ya mapema hujaribiwa na kuthibitishwa.
Hivi sasa, kazi zote za uhandisi wa ujenzi kama vile kingo za barabarani, madaraja, mikondo ya barabara na mahandaki zimekamilika. Maandalizi ya uendeshaji yanafanywa kwa utaratibu.
Baada ya kukamilika kwa kazi ya pamoja ya uthibitishaji na majaribio, uendeshaji zaidi wa majaribio na tathmini za usalama zitafanywa kabla ya kuanza rasmi uendeshaji wa reli hiyo.
Njia hiyo ya reli ya mwendo kasi, ambayo ni mradi wa kihistoria chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililopendekezwa na China, inaunganisha mji mkuu wa Indonesia, Jakarta na mji mwingine mkubwa wa Bandung.
Ikiwa imeundwa kuendeshwa kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa, reli hiyo yenye urefu wa kilomita 142.3 itapunguza muda wa safari kati ya Jakarta na Bandung kutoka zaidi ya saa tatu hadi dakika 40 hivi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma