

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kwa serikali, wadau binafsi kuchukua hatua za ujasiri kwa mustakabali endelevu wa Dunia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 17, 2023. (Xinhua/Xie E)
Huang Runqiu (wa nne kulia), Mkuu wa COP15 na Waziri wa Ikolojia na Mazingira wa China, na Elizabeth Maruma Mrema (wa pili kulia), Katibu Mtendaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, wakipiga makofi baada ya kupitishwa kwa Mfumokazi wa Kimataifa wa Bioanuwai wa Kunming-Montreal katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa bioanuai, COP15, huko Montreal, Canada, Desemba 19, 2022. (Xinhua/Lian Yi)
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatatu alitoa mwito kwa serikali na wadau binafsi duniani kote kuimarisha kujitolea kwao na kuchukua hatua madhubuti za kujenga mustakabali endelevu wa Dunia.
"Makubaliano ya mwaka jana ya Kunming-Montreal juu ya Mfumokazi wa Dunia wa Bioanuai yaliashiria hatua muhimu -- lakini sasa ni wakati wa kutoka kwenye makubaliano hadi hatua," afisa huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika ujumbe wake wa video kwa Siku ya Kimataifa ya Bioanuwai, ambayo huadhimishwa Mei 22 kila mwaka.
"Hii inamaanisha kuhakikisha uzalishaji na mifumo ya matumizi ambayo ni endelevu, kuelekeza ruzuku kutoka kwenye shughuli za uharibifu wa mazingira asilia kuelekea suluhisho za kijani, kutambua haki za watu wa kiasili na jamii za wenyeji, walinzi hodari wa bioanuwai ya Dunia yetu, na kusukuma serikali na kampuni kuchukua hatua kali na za haraka dhidi ya upotevu wa bioanuai na athari za tabianchi," amesema.
Guterres ameonya kwamba vitendo vya binadamu vinaharibu kila kona ya sayari na "spishi milioni 1" ziko katika hatari ya kutoweka kutokana na uharibifu wa makazi, uchafuzi wa mazingira na hali mbaya ya tabianchi.
Ametoa wito kwa binadamu "kumaliza vita hivi dhidi ya mazingira ya asili."
"Hebu tufanye kazi kwa pamoja katika serikali, mashirika ya kiraia, na sekta binafsi ili kupata mustakabali endelevu kwa wote," amesema mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
Siku ya Kimataifa kwa ajili ya Bioanuwa ni siku iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhimiza masuala ya bioanuwai.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma