Balozi mpya wa China nchini Marekani ahimiza uhusiano wa nchi hizo mbili kurudi kwenye njia sahihi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 24, 2023
Balozi mpya wa China nchini Marekani ahimiza uhusiano wa nchi hizo mbili kurudi kwenye njia sahihi
Xie Feng, Balozi mpya wa China nchini Marekani akitoa maelezo mafupi kwa vyombo vya habari alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy mjini New York, Marekani, Mei 23, 2023. Xie Feng ameitaka Washington kufanya kazi na China kuimarisha mazungumzo, kudhibiti tofauti na kukuza ushirikiano, ili kuufanya uhusiano wa China na Marekani kurudi kwenye njia sahihi. (Xinhua/Li Rui)

NEW YORK - Xie Feng, Balozi mpya wa China nchini Marekani, Jumanne ameitaka Washington kufanya kazi na China ili kuimarisha mazungumzo, kudhibiti tofauti na kukuza ushirikiano, ili kuufanya uhusiano wa China na Marekani kurudi kwenye njia sahihi.

"Nina heshima kubwa kuteuliwa na Rais Xi Jinping kuwa Balozi wa 12 wa China nchini Marekani," amesema Xie katika hotuba yake fupi kwa vyombo vya habari alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy Jumanne mchana.

"Kama mwakilishi wa watu wa China, nimekuja hapa ili kulinda maslahi ya China, na ninalichukulia hili kama jukumu langu takatifu. Kama mjumbe wa watu wa China, nimekuja hapa ili kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Marekani na ninachukua hii kama dhamira yangu muhimu," Xie amesema.

"Kwa sasa uhusiano kati ya China na Marekani unakabiliwa na matatizo na changamoto kubwa. Uteuzi wangu kwangu unamaanisha si tu heshima, bali pia ni wajibu mkubwa. Mimi na wenzangu tutatekeleza wajibu wetu na kutekeleza wajibu wetu kwa bidii na ujasiri, Xie amesema.

Amesema kuwa, Rais Xi Jinping ameweka mbele kanuni tatu za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana, ambazo zinawakilisha njia ya msingi na sahihi kwa nchi hizo mbili kwenda pamoja kwa kupatana katika zama mpya.

"Tunatumai kuwa Marekani itaenda katika mwelekeo mmoja na China, na kuchukua hatua kwa maslahi ya pamoja ya watu wa nchi hizi mbili na Dunia, kushughulikia ipasavyo masuala muhimu na nyeti, kama vile suala la Taiwan kwa kufuata kanuni za taarifa tatu za pamoja za China na Marekani," ameongeza.

"Imepita miaka 13 tangu nilipofanya kazi Marekani mara ya mwisho. Katika miaka 13 hiyo iliyopita, Dunia imepitia mabadiliko makubwa, na Marekani pia," Xie amesema.

"Katika muda wangu wa kuwa balozi, ninatarajia kuwasiliana na watu wa Marekani kutoka kada zote za maisha, kutazama na kuijua nchi hii kwa ukaribu, na kutafuta njia za kuimarisha mawasiliano na ushirikiano," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha