

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Algeria asema Timu ya Madaktari wa China imetoa mchango mkubwa kwa huduma ya afya ya Algeria
Balozi wa China nchini Algeria Li Jian akihutubia kwenye hafla iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini Algeria kusherehekea mwaka wa 60 tangu kutumwa kwa timu za madakari wa China nchini Algeria mjini Algiers, Algeria Mei 21, 2023.
Tangu Mwaka 1963, China imetuma vikundi 27 vya timu za madaktari nchini Algeria, kutibu wagonjwa wapatao milioni 27.37, kufanya upasuaji takriban milioni 1.75 na kusaidia akina mama wajawazito kujifungua watoto wachanga wapatao milioni 2.07. (Xinhua)
Li Bin, Mkuu wa Shirikisho la Urafiki wa Watu wa China na Afrika, akihutubia hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya kutumwa kwa timu za madaktari wa China nchini Algeria iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini Algeria mjini Algiers Tarehe 21 Mei, 2023. (Xinhua)
Mohamed Talhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Algeria, akihutubia hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya kutumwa kwa timu za madaktari wa China nchini Algeria iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini Algeria mjini Algiers Tarehe 21 Mei, 2023. (Xinhua)
ALGIERS - Ubalozi wa China nchini Algeria Jumapili ulisherehekea maadhimisho ya mwaka wa 60 tangu kutumwa kwa timu za madaktari wa China nchini Algeria.
Mohamed Talhi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Algeria, ameishukuru timu ya madaktari wa China kwa mchango wao katika maendeleo ya afya nchini Algeria.
Talhi amesema tangu China ilipotuma timu yake ya kwanza ya madaktari nchini Algeria Mwaka 1963, wahudumu wa afya wa China wamefanya kazi pamoja na madaktari wa Algeria kutoa huduma za matibabu kwa Waalgeria.
Talhi pia ameishukuru China kwa msaada wake mkubwa kwa taasisi za matibabu za Algeria katika suala la huduma za kujitolea na vifaa vya matibabu.
Li Bin, Mkuu wa Shirikisho la Urafiki wa Watu wa China na Afrika, amesema kazi za timu ya madaktari wa China nchini Algeria zinaonyesha kikamilifu kuaminiana kwa pande zote na urafiki wa dhati kati ya watu wa nchi hizo mbili, na imekuwa mfano wa ushirikiano wa China na Algeria.
Balozi wa China nchini Algeria Li Jian amesema, katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, timu za madaktari wa China zimechangia katika huduma ya afya ya umma ya Algeria, ushirikiano wa afya kati ya nchi hizo mbili na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Yang Yong, mkuu wa kundi la 27 la timu ya madaktari wa China nchini Algeria, amesema kuwa madaktari wa China nchini Algeria wataendelea kubuni njia mpya za kutoa msaada wa kimatibabu, huku wakionyesha teknolojia mpya, mbinu mpya na mawazo mapya.
Tangu Mwaka 1963, China imetuma vikundi 27 vya timu za madaktari nchini Algeria, kutibu wagonjwa wapatao milioni 27.37, kufanya upasuaji takriban milioni 1.75 na kusaidia akina mama wajawazito kujifungua watoto wachanga wapatao milioni 2.07.
Habari Picha: Mandhari ya maeneo yanayozunguka Mto Bahe katika Mji wa Xi'an, China
Katika Picha: Watu wakivuna matunda ya bluberi katika Kijiji cha Wengbao, Mkoa wa Guizhou wa China
Habari Picha: Ndege wakionekana Lhasa, huko Tibet, Kusini Magharibi mwa China
Katika Picha: Tazama mandhari ya Mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma