Kampuni ya kuunda mabasi ya China yazindua mabasi ya kwanza yanayotumia umeme nchini Nigeria

(CRI Online) Mei 24, 2023

Kampuni ya kuunda mabasi ya China, Yutong, jana Jumanne imezindua mabasi ya kwanza yanayotumia umeme kwa ajili ya usafiri wa umma mjini Lagos, Nigeria, wakati nchi hiyo ikijiandaa kuachana na mabasi yanayotumia nishati ya mafuta na kuanza kutumia magari yanayotumia nishati ya umeme.

Mradi huo ni uratibu wa pamoja kati ya kampuni ya Oando Clean Energy, ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya Yutong nchini Nigeria, na Mamlaka ya Uchukuzi ya mji wa Lagos, na umeanza kwa mabasi mawili yanayotumia umeme ya Yutong katika barabara ya mabasi ya mwendokasi mjini Lagos.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Gavana wa Lagos Babajide Sanwo-Olu amesema, hatua hiyo inaendana na malengo ya mji huo kuwa mji wa kisasa. Pia amesema, mfumo wa usafiri wa umma nchini Nigeria unataka kuchukua jukumu chanya katika kupunguza utoaji wa hewa chafu, na kuongeza kuwa mabasi hayo mapya yanayotumia umeme yatapunguza utoaji wa hewa chafu na pia kuongeza ufanisi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha