Tanzania kualika mwekezaji wa kimataifa kuchukua uendeshaji wa shughuli za bandari

(CRI Online) Mei 25, 2023

Serikali ya Tanzania imetangaza mipango ya kuanzisha mchakato wa kumpata mwekezaji wa kimataifa mwenye uwezo kushughulikia uendeshaji wa bandari kuu ya Dar es Salaam nchini humo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa ameliambia bunge kuwa mwekezaji anayependekezwa anatakiwa kufikia vigezo vya kimataifa ili kuifanya bandari hiyo kuwa na ushindani zaidi.

Mbarawa ametangaza mchakato huo jumanne baada ya wabunge kuitaka serikali kubinafsisha uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi wake.

Kwa mujibu wa Waziri Mbarawa, mwekezaji huyo anapaswa kuwa na kampuni ya kimataifa yenye mtandao sahihi na uzoefu mkubwa katika sekta ya uchukuzi wa majini, na pia mwenye uwezo wa kupata masoko mapya.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha