

Lugha Nyingine
Reli ya Ethiopia-Djibouti yaanza usafirishaji wa malori
Reli inayounganisha nchi za Ethiopia na Djibouti iliyojengwa na China jana jumatano imeanza kusafirisha malori kutoka bandari za nchini Djibouti kwenda katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Shehena ya kwanza ya malori 63 iliwasili jana jumatano katika Kituo cha Mizigo cha Indode, pembezoni mwa mji wa Addis Ababa, ambapo hafla maalum ilifanyika kituoni hapo kuashiria kuwasili kwa shehena hiyo.
Waziri wa Nchi anayeshughulikia Uchukuzi na Ugavi, Denge Boru, ameelezea hatua hiyo kuwa ni muhimu katika lengo la Ethiopia la kuboresha sekta ya uchukuzi na ugavi. Pia amesisitiza umuhimu wa mchango mkubwa wa usafiri wa reli katika kuboresha biashara ya ndani na nje ya nchi hiyo.
Waziri huyo amesema, usafiri na ugavi ni sehemu muhimu za matarajio ya serikali ya Ethiopia katika kuleta maendeleo ya jamii na uchumi, ambapo reli inachukua nafasi muhimu katika mageuzi ya sekta hiyo.
Habari Picha: Mandhari ya maeneo yanayozunguka Mto Bahe katika Mji wa Xi'an, China
Katika Picha: Watu wakivuna matunda ya bluberi katika Kijiji cha Wengbao, Mkoa wa Guizhou wa China
Habari Picha: Ndege wakionekana Lhasa, huko Tibet, Kusini Magharibi mwa China
Katika Picha: Tazama mandhari ya Mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma