Rais wa China apongeza walimu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Macau

(CRI Online) Mei 26, 2023

Rais wa China Xi Jinping wiki hii ametuma barua kwa wawakilishi wa walimu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Macau wa China walioshiriki kwenye utafiti na maendeleo ya setilaiti za anga ya juu za “Macao Science 1”, akiwapongeza na kuwatia moyo.

Katika barua yake, Rais Xi amesema, ameona kidhahiri ari na uwajibikaji wa wanafunzi hao katika maendeleo ya sayansi na teknolojia na kujenga nguvu ya China katika anga ya juu.

Rais Xi pia amesema, kuimarishwa kwa ushirikiano wa kiteknolojia kati ya Macau na China Bara katika maeneo kama anga ya juu katika miaka ya karibuni kumepata matokeo makubwa. Ameeleza matumaini yake kuwa, kitivo hicho kitaendeleza utamaduni mzuri wa kupenda nchi na Macau, kujumuisha maendeleo ya Macau katika maendeleo ya taifa, kuchukua nafasi dhahiri katika maendeleo ya Eneo la Ghuba ya Guangdong-Hong Kong-Macau, na kusaidia juhudi za Macau kupanua uchumi wake ili kutoa mchango mpya katika mafanikio ya kanuni ya ‘nchi moja, mifumo miwili’ mkoani Macau.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha