Umoja wa Mataifa watoa heshima kwa walinda amani waliouawa wakiwa kwenye majukumu yao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kulia) akihutubia shughuli yenye kichwa kisemacho "Hafla ya Medali ya Dag Hammarskjold na Tuzo ya Mtetezi Bora wa Kijeshi wa Jinsia" kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 25, 2023. (Evan Schneider/Picha ya UN/ Kutumwa Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Umoja wa Mataifa umefanya shughuli kwenye makao yake makuu mjini New York siku ya Alhamisi, kuenzi kumbukumbu ya walinda amani waliojitolea maisha yao wakati wakiwa kwenye majukumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameweka shada la maua kwenye Kumbukumbu ya Walinda Amani kwa heshima ya walinda amani zaidi ya 4,200 wa Umoja huo ambao wamepoteza maisha tangu Mwaka 1948.

Muda mfupi baadaye, aliongoza hafla katika Ukumbi wa Mkutano Mkuu ambapo Medali za Dag Hammarskjold zilitunukiwa baada ya vifo vya wanajeshi, polisi na walinda amani wa kiraia 103 ambao walipoteza maisha yao wakiwa kwenye majukumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa mnamo Mwaka 2022.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Guterres amesema kwa raia walionaswa katika vita, helemeti za buluu za Umoja wa Mataifa zinazounga mkono usalama, utulivu na utawala wa sheria katika nchi zinazowakaribisha zinaonekana kama "mnara wa matumaini na ulinzi."

"Wanawakilisha moyo unaodunda wa kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kwa amani," amesema. "Kwa kuleta pamoja walinda amani kutoka duniani kote, ulinzi wa amani pia umekuwa ishara ya msukumo wa ushirikiano wa pande nyingi katika vitendo."

Hafla hiyo ya Alhamisi imeandaliwa ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa, ambayo itaadhimishwa Mei 29, na kuadhimisha miaka 75 ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.

Ujumbe wa kwanza wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ulianzishwa Mei 1948, wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipoidhinisha kutumwa kwa idadi ndogo ya waangalizi wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati ili kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la Usimamizi wa Usimamishaji Vita kufuatilia Mkataba wa Silaha kati ya Israeli na nchi jirani zake za Kiarabu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa kwa vyombo vya habari, zaidi ya walinda amani milioni 2 kutoka nchi 125 wamehudumu katika operesheni 71 duniani kote. Leo, wanawake na wanaume 87,000 wanahudumu katika maeneo 12 yenye migogoro barani Afrika, Asia, Ulaya na Mashariki ya Kati.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kwenye mimbari na skrini) akihutubia shughuli yenye kichwa kisemacho "Hafla ya Medali ya Dag Hammarskjold na Tuzo ya Mtetezi Bora wa Kijeshi wa Jinsia" kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 25, 2023. (Evan Schneider/Picha ya UN/ Kutumwa Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha